Mtandao upi wa simu una huduma bora na za uhakika?

Forgotten

JF-Expert Member
Jul 20, 2018
3,467
10,714
Hii mitandao ya simu Tanzania imekuwa kero sasa, unajikuta una laini ya kila mtandao na kila laini unasajili kwa kazi yake kwasababu hakuna mtandao unaotoa huduma zake kwa 100%.

Nina laini za mitandao mitano lakini kila mmoja una matatizo yake.

Halotel, laini yao imeacha kufanya kazi ghafla tu, ni wiki sasa. Ukiwa na salio la muda wa maongezi wanakata, ukiwapigia wanaanza kululazimisha ulijiunga kwenye huduma ambazo hata huzijui. Kiufupi ni wezi.

Airtel, kwenye Internet ni 0 kabisa, unajiunga bundle, speed ya kobe lakini bundle linatembea kwa kasi ya 5G.

TTCL, huduma zao ni hovyo, T-Pesa haina uhakika, laini yao inapokea sms zote ila siyo za miamala au vifurushi.

Tigo, laini yao nilivunja kabla hata hawajawapa Yas kampuni, mtandao wa hovyo kuwahi kutokea TZ.

Vodacom, wanajifanya wazungu ila nao wameanza kuwa waswahili. Angalau kwenye Unlimited Internet wanajitahidi.
 
Niko maeneo ya Buswelu Ilemela Mwanza na nina line za mitandao ya Vodacom, Airtel, Yas na Halotel na ziko hewani.
Hapa Vodacom ina afadhali kuliko mitandao mingine yote; japo kwa asilimia 50 mpaka 60 kwa Huduma za Sauti na Internet. Mitandao mingine ufanisi wake uko chini ya asilimia 50; kwa maoni yangu kama ifuatavyo:-
Airtel 30 - 40%
Yas 30 - 35%
Halotel 25 - 30%
Mabadiliko makubwa ya teknolojia yanapaswa kufanyika ili kunusuru uwezo wa mitandao Tanzania.
 
Hakuna unafuu wa mitandao,wiki iliyopita nilikuwa nataka kutoa ela kwa mpesa,kila nikitoa inagoma mpaka wakala akawa anaanza kuwa na wasi wasi na mimi alafu kuna jamaa inabidi nimlipe fasta atembee usafiri umemsubiria,ilikuwa mbaya sana hii kwangu ni aibu
 
Pole sana mkuu huduma za mawasiliano bado changamoto kubwa sana
Hakuna unafuu wa mitandao,wiki iliyopita nilikuwa nataka kutoa ela kwa mpesa,kila nikitoa inagoma mpaka wakala akawa anaanza kuwa na wasi wasi na mimi alafu kuna jamaa inabidi nimlipe fasta atembee usafiri umemsubiria,ilikuwa mbaya sana hii kwangu ni aibu
 
Back
Top Bottom