Influenza
JF-Expert Member
- Jul 1, 2018
- 1,489
- 3,643
Katika Mtaala wa Elimu wa Kidato cha V na VI 2023 umefanya mabadiliko ya Tahasusi ambapo Tahasusi katika Kidato cha V na VI zimegawanywa katika maeneo saba ya ujifunzaji ya Sayansi ya Jamii, Lugha, Elimu ya Biashara, Sayansi, Michezo, Sanaa na Elimu ya Dini.
Idadi na aina ya tahasusi zitapitiwa mara kwa mara kuhakikisha zinakidhi mahitaji halisi ya Taifa katika wakati husika.
Ili kuongeza wigo wa fursa za kujiunga na elimu ya juu, idadi ya masomo katika kila tahasusi haitakuwa chini ya matatu na haitazidi manne kulingana na uwezo na malengo ya mwanafunzi.
Aidha, aina ya masomo katika kila tahasusi, imezingatia malengo ya kitaalamu (career aspirations and pathways) ya wahitimu na rasilimali zitakazokuwepo shuleni.
Pia, mwanafunzi wa Elimu ya Sekondari Kidato cha V na VI ataruhusiwa kuchagua masomo ya ziada, yakiwemo yale ya Mkondo wa Elimu ya Amali, kulingana na ratiba na uwezo wa shule husika ili kujiongezea umahiri utakaomwezesha kumudu maisha yake baada ya kuhitimu.
Soma Mtaala Mzima hapa;