Msuya na Warioba: Tatizo la dira 2050 ni siasa

Kamundu

Platinum Member
Nov 22, 2006
7,276
9,973
Mawaziri wazee wetu wastaafu wote Warioba na Msuya wamesema tatizo kubwa la Dira yetu ya taifa ni kutokuwa na mfumo wa siasa wa kueleweka.

Kwa muda mrefu sasa tumekuwa na mifumo ya vyama vingi lakini wakati huohuo serikali hiyo hiyo ndiyo wanaongoza kuharibu chaguzi zetu na kusumisha mfumo wa demokrasia. Hii ni kuwa na mfumo ambao hatujui kama tunataka mfumo wa aiana gani. Hatuwezi kuweka mipango ya miaka 50 bila kuwa na dira iliyo nyooka ya siasa na mifumo yake. Huwezi kuchagua mfumo ambao serikali yenyewe haiwezi kutekeleza.

Tatizo la pili kubwa ni Zanzibar. Katiba yetu ikifuatwa vizuri haitambui kabisa katiba ya Zanzibar hivyo ni katiba ambayo kisheria haitambuliki na hii ya Muungano. Huwezi kuwa na nchi mmoja na katiba mbili! Labda tusema kwa uwazi kwamba katiba ya Tanganyika ndiyo ya Tanzania.

Tatizo kubwa hatuna viongozi wazalendo wa kweli ambao hawajali vyama wanajali nchi. Angalieni wenzetu kama Kenya pamoja na ukabila wao wanehakikisha kuna katiba nzuri na hawaogopi kushindana hata kama kiongozi anasinda kwa 1% anaheshimiwa kwasababu wamekubali mfumo. Watanzania hasa CCM wanapeleka mbele bila kujua matatizo yata ongezeka zaidi kwa viongozi wa huko mbele.
 
Ukiwa ndani huwezi kujua kama nje kuna giza maana muda wote taa zimewashwa ILA ukitoka ndani ndipo utajua kuna giza.
 
Katiba iwe Ile ya Warioba
 
Back
Top Bottom