Mstahiki Ramadhani Kapera Meya wa Tabora usitumie ubabe wajibu wananchi wako

Hismastersvoice

JF-Expert Member
Jan 26, 2013
21,182
25,970
Mstahiki Meya dhamana uliyopewa kuiongoza manispaa ya Tabora usiigeuze fimbo ya kuwachapia wakazi wako. Mkazi mtu mzima alikuuliza swali kuhusu wale mnaowaajiri kwa kujuana na kuwapa kazi mishahara na vifaa vya usafi wa mitaro wako wapi mpaka muwalazimishe wakazi kufanya kazi hizo pasipo na vifaa?

Mstahiki Meya badala ya kumjibu huyo mzee unaamuru ambaye hatafanya usafi atozwe faini ya shilingi elfu hamsini, kwako wewe ni vijisenti tu chini ya robo ya posho yako ya siku usilolijua ni kuwa huyo mwananchi hana uwezo wa kupata milo miwili kwa siku.

Mwananchi huyo alikutajia tozo mnazowatoza kama kodi ili manispaa iwahudumie, lakini badala ya kuwahudumia mnawalipa mishahara vijana wenu mlio waajiri bila kufanya kazi wanazotakiwa wazifanye, kitendo chako ni kuwanyima haki yao ya matumizi ya kodi wanazolipa.

Mhe. Ramadhani ninakutakia Ramadhan njema.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom