Msimu wa kero ya michango ya harusi umewadia, Umejiandaaje?

Mwanga Lutila

JF-Expert Member
Nov 10, 2016
4,138
13,826
Wasalaam,


Miezi ya 4 mpaka wa 10 ndio miezi ya watu kufunga ndoa na pilika pilika za harusi.
Na ndio miezi ambayo huwa na ugomvi na kuchukiana kwa sababu ya wingi wa Kadi za harusi mpaka inageuka kuwa kero, mtu mmoja ambaye ni wa 'kucheka cheka na watu' anajikuta ana kadi za harusi zaidi ya tano.

Mimi binafsi mpaka sasa nina kadi nne, Kadi moja ni ya Sendoff, mchango Elfu hamsini, Kadi tatu za harusi mbili ni Elfu hamsini na nyingine Laki.
Na mwingine aliniletea huyu naye ilikuwa Laki moja, nikamwambia Bwana Chukua hii Elfu 20 itawasaidia kuongeza bajeti na kadi yako nenda nayo maana hali ni ngumu.


Hawa wengine sikuweza kuwakatalia kwasababu ni 'wanyalukolo' hivyo ingepelekea kununiwa mwaka mzima.

Kwa kifupi huu ndio muda wa kero za michango kuanza. Wengine unaweza kuwakwepa na wengine huwezi kuwakwepa.
 
Uko sahihi binafsi nina kadi nne zote za mwezi June.
 
Kwangu yule aliyenichangia tu ndo ataiona hela yangu na kwa kiwango kile kile sio tofauti na hivyo,sometimes huwa hata najuta kwanini niliwachangisha watu maana kuna wakati zinagongana kadi inatakiwa ndani ya miezi minne nitoe 500,000/=na hali hii ya Magu unaweza kugoma kutoa ukaonekana m'baya.
 
1.Nina kadi ya harusi ya czn wangu tarehr 29/4
2.Nina kadi ya harusi ya kaka wa baba mdogo tarehe 15/ 5
3. Nina kadi ya mtoto wa mjomba anaowa tarehe 29/5
4. Nipo kwenye kamati ya kaka yangu toka ni toka anaowa tare 10/6
5. Staff mwenzetu katupa kadi ndoa mwez 7
6. Staff mwingine send off wiki ya kwanza ya mwez wa 7

7 . Nipo katibu wa kamati ya harusi ya rafiki yangu kipenz mwez wa 8, tunaanza kikao cha
Kwanza after pasaka...

Mshahara wangu take home laki 5.. nisaidieni nafanyaje....
 
kuna mmoja baba mama kaka mdogo wanakubusha mchango wa harusi haloo sipumui nimekasirika nikasema na sichangii si kwa sms zile kila baada ya siku tatu
 
changa ule nyasi
 
Nina bahati ya kupishana nazo sana.
Wakizileta nazipokea halafu nazipotezea.
Akinuna shauri yake.
Maisha ameyataka mwenyewe halafu awasumbue wengine?
Wakishaoana huwaoni.
Hachangii mtu hapa.
 
Jinyonge
 
Jiteke na kujiumiza. Watakuchangia kwa janga hilo halafu nawe unawachangia kimtindo.
 
Ni mt'hani mzito na wote ndugu hukuchanga unaambiwa una dharau kazi nzuri unayo{ndivyo wanavyoamini}ila shughuli za kifamilia unajitenga,hamna namna mkuu ahidi kiasi kidogo cha pesa utakachomudu kwa kila mmoja wakihoji waambie ukweli kuwa hali mbaya.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…