Kikiwa chama kikubwa zaidi cha siasa duniani ambacho kina wanachama zaidi ya milioni 96, CPC kinatawala nchi yenye watu zaidi ya bilioni 1.4. Kutokana na uongozi mtulivu wa muda mrefu na thabiti wa Chama hicho, China imepata mafanikio ya kushangaza katika ustawi wa watu. Mwaka 1949 ambao ni mwaka Chama hicho kilianza kutawala China, pato la taifa la China lilikuwa asilimia 7.6 tu ya lile la Marekani, lakini mwaka 2021 kiwango hicho kiliongezeka hadi asilimia 77.1, ikiwa ni ongezeko la zaidi ya mara kumi.
China imeshinda vita kubwa zaidi ya kupunguza umaskini katika historia ya binadamu, na kuondoa kabisa tatizo la umaskini uliokithiri nchini humo. China pia imetoa bima ya matibabu kwa watu bilioni 1.36, na bima ya kimsingi ya uzeeni kwa zaidi ya watu bilioni 1. Nchini China, asilimia 95.4 ya watu wamepata elimu ya lazima ya miaka 9, na asilimia 57.8 wamepata elimu ya juu. Mwaka 2021, wastani wa umri wa kuishi wa Wachina ulifikia miaka 78.2, na kiwango hicho kimeshinda nchi nyingi zilizoendelea.
Kuzingatia watu zaidi pia kunaoneshwa katika kuwajibika kwa maisha na afya ya watu. Katika miaka mitatu iliyopita tangu kulipuka kwa janga la UVIKO-19, China imechukua hatua madhubuti zaidi za kukabiliana na virusi, ili kuhakikisha afya na usalama wa maisha ya watu.
Katika Mkutano Mkuu wa 20 wa Wajumbe Wote wa CPC, Chama hicho kimefafanua jukumu kuu katika kipindi kijacho, ambalo ni “kuungana na kuwaongoza watu wa makabila yote nchini China ili kujenga nchi yenye nguvu ya kisasa ya kijamaa katika pande zote, kutimiza lengo la pili la miaka mia moja, na kusukuma mbele ustawi wa taifa la China kwa njia ya kisasa ya Kichina”. “Nchi ni watu, na watu ni nchi,” maneno haya ya rais Xi kwa mara nyingine tena yameonesha lengo kuu la CPC ni kuwawezesha Wachina wote kuwa na maisha bora.
Kuzingatia zaidi watu ni hitaji la ujenzi wa Ujamaa Maalum wa Kichina katika zama mpya. CPC kwa kuchukulia Mkutano Mkuu wa 20 kama mwanzo mpya, kitaongoza watu wa China kutimiza mafanikio makubwa zaidi katika mchakato wa kupata maisha bora.