Analogia Malenga
JF-Expert Member
- Feb 24, 2012
- 5,106
- 10,178
Serikali ya Ethiopia imeahidi kukarabati Msikiti wa kale wa uliyoharibiwa mwezi uliyopita katika mzozo uliyokumba jimbo la Tigray kaskazini mwa nchi hiyo
Msikiti wa al-Nejashi uliripotiwa kushambuliwa kwa makombora, vitu ndani kuibwa na makaburi ya kihistoria ya viongozi wa Kiislamu kuharibiwa.
Serikali ilisema Kanisa lililoharibiwa wakati wa mzozo huo pia litakarabatiwa.
Wakazi wanaamini Msikiti wa al-Nejashi ulijengwa na Waislamu wa kwanza kuhamia Afrika enzi ya Mtume Muhammad.
Walikuwa wamekimbia mateso huko Makka na wakapewa hifadhi katika uliokuwa Ufalme wa Aksum.
Waislamu katika eneo hilo wanaamini kwamba maswahaba 15 wa Mtume Muhammad walizikwa katika makaburi yaliyoharibiwa.
Pia wanasema Msikiti huo ni wa kale zaidi Afrika, japo wengine wanaamini uko Misri.
Msikiti huohuo katika mji wa Wukro, karibu kilomita 800 (miili 500) kutoka mji mkuu wa Ethiopia, Addis Ababa.
Kanisa la Wakristo wa Orthodox, wa Saint Emmanuel, Pia uliharibiwa lakini hakuna maelezo yaliyotolewa.
Mwaka 2015 Shirika la misaada la Uturuki ulilizindua mradi wa kuukarabati Msikiti huo, na kuongeza kuwa lilitaka ''kuhifadi turathi'' hiyo ya kale na kufanya eneo hilo kuwa kivutio cha ''Utalii wa kidini''.
Shirika lisilo la kiserikali la Ubelgiji, linaloendesha shughuli zake Afrika, mnamo Desemba 18 liliripoti kwamba Msikiti wa al-Nejashi "ulilipuliwa kwa bomu kwanza na baadaye kuporwa na wanajeshi wa Ethiopia na Eritrea".
" Vyanzo via habari ndani ya Tigray zinasema kwamba watu kadhaa walifariki wakijaribu kulinda Msikiti huo," iliongezza ripoti hiyo.
Serikali haijatoa tamko lolote kuhusiana a na repoti hizo. Serikali zote za Ethiopia na Eritrea pia zinakanusha kuwa vikosi vya Eritrea viko Tigray kusaidia katika vita dhidi ya TPLF.
Jumatatu, televisheni ya serikali ya Ethiopia ilinukuu wakazi wakisema kwamba vikosi vya TPLF vilichimba mitaro kuzunguka msikiti huo, bila kutoa maelezo zaidi.
Serikali imeweka vikwazo vikali dhidi ya vyombo vya habari kuripoti kuhusu hali ilivyo ndani ya Tigray, na kufanya kuwa vigumu kubaini ni lini vikwazo hivyo vitaondolewa.
Wafanyakazi wa kutoa misaada pia wamedhibitiwa kuingia Tigray.
Katika mahojiano na BBC Idhaa ya Amharic, Naibu Mkurugenzi wa Mamlaka ya kuhifadhi maeneo ya kale, Abebaw Ayalew, alisema kamati maalum itapelekwa kutathmini kiwango cha uharibifu dhidi ya Msikiti na Kanisa kabla shughuli ya ukarabati kuanza .
"Maeneo haya sio ya kuabudu pekee, Bali pia ni turathi ya kale kwa Ethiopia nzima,"alisema.
Mzozo huo ni mbaya kiasi gani?
Hijabainika ni watu wangapi waliuawa katika mzozo huo lakini Bw. Abiy aliwahi kusema wanajeshi hawakuua raia hata mmoja wakati wa oparesheni iliyochangia kuondoa madarakani TPLF.UN na mashirika mengine ya kutetea haki yametoa wito wa kufanyika uchunguzi huru kuhusiana na madai yanayotolewa na pande zote ikiwa ni pamoja na mauaji ya raia, mashambulio ya mabomu na uporaji wa maeneo ya makazi ya watu na hospitali.
Zaidi ya watu 50,000 wamekimbilia Sudan kutoroka mapigano.
Mapigano yalisababishwa na nini?
Mzozo ulizuka mapema mwezi Novemba, wakati Waziri Mkuu wa Ethiopia Abiy Ahmed alipoamuru oparesheni ya kijeshi dhidi vikosi vya Tigray.Alisema amechukua hatua hiyo kujibu mashambulio dhidi ya kambi ya majeshi ya muungano ndani ya jimbo la Tigray.
Mzozo uliibuka baada ya miezi kadhaa ya mvutano kati ya serikali ya Bw. Abiy na viongozi wa TPLF - Chama tawala katika jimbo la Tigray.
Kwa karibu miongo mitatu, chama hicho kilikuwa uongozini kabla ya kuwekwa kando Bw. Abiy alipoingia madarakani mwaka 2018 wakati wa maamndamano makali ya kupinga serikali.