Prof Janabi wa JF
Senior Member
- Jul 7, 2023
- 142
- 417
Wala siwezi kuwa kama wengine wanaowatisha watu kuwa huku maisha magumu. Mgumu ni wewe. Vitisho mnavyosikia kuwa maisha ya Marekani ni magumu, ni sawa na vitisho vya watu wa Dar kwa watu wa mkoani kuwa Dar maisha magumu. Ila kiukweli ukienda Dar ukiwa na mishe za kufanya, mambo ni mepesi tu.
Niko US kwa kitambo sasa, na niponipo sana. Nimeona watu wengi wanawaambia watu mbaki nyumbani msije huku, aisee msikubaliane na hilo, pambaneni mje muone mambo. Hata hivyo msije kama wanaoenda Dar kwa mbio za Mwenge.
Ushauri wangu wa namna nyepesi ya kuja huku ni safari za kielimu, vipaji na kazi. Vipaji vitakuweka kwa muda mfupi, ila elimu na kazi vinaweza kukuweka muda mrefu sana hadi ukapata kujua namna ya kufanya maajabu.
US sio kugumu, wagumu ni nyie, maisha ni mteremko, kila kitu kinapatikana hadi nanii.. kazi ni kwenu.
Karibuni sana Marekani.
Nasisitiza, nitatamba sana.