Setfree
JF-Expert Member
- Dec 25, 2024
- 2,645
- 3,590
Watu wengi wamejaa fadhaa kutokana na mambo mbalimbali yanayoendelea huku na kule duniani: vita, magonjwa ya kutisha, ukosefu wa ajira, njaa, uhalifu, matetemeko, gharama kubwa za maisha, nk.
Rafiki, usifadhaike. Hayo yote karibu yatakwisha. Biblia inatuhakikishia kuwa hayo si maisha ya milele. Mungu anaumba dunia mpya isiyo na maovu, mateso wala huzuni.
“Sasa, naumba mbingu mpya na dunia mpya, mambo ya zamani hayatakumbukwa tena. Furahini, mkashangilie milele, kwa ajili ya vitu hivi ninavyoumba.."(Isaya 65:17)
Katika mbingu mpya na dunia mpya:
Hakutakuwa na machozi tena wala maombolezo au kilio. (Ufunuo 21:4)
Hakutakuwa na magonjwa wala mauti. Haki itatawala, na amani itakuwa ya kudumu.
"Lakini, kulingana na ahadi yake, twatazamia mbingu mpya na nchi mpya, ambayo haki yakaa ndani yake."(2 Petro 3:13).
Hayo sio maneno ya kukutia moyo tu, ni ahadi za kweli kutoka kwa Mungu ambaye hasemi uongo. Kwahiyo tunapoona mambo yanazidi kuwa mabaya duniani, ni ishara kuwa mwisho wa mambo hayo umekaribia.
"Basi mambo hayo yaanzapo kutokea, changamkeni, mkaviinue vichwa vyenu, kwa kuwa ukombozi wenu umekaribia."(Luka 21:28)