Msemaji Mkuu wa Serikali: Barabara za Kimara, Mbagala zitapata Mabasi mapya ya Mwendokasi kati ya Februari au Machi 2025

Mtoa Taarifa

JF-Expert Member
Sep 21, 2024
211
661
Msemaji Mkuu wa Serikali, Gerson Msigwa, amesema mradi wa Mabasi yaendayo Kasi unatarajia kupokea Mabasi mapya kuanzia mwezi wa Pili hadi wa Tatu mwaka 2025

Akizungumza leo Januari 2, 2025 amesema "Tayari kuna Mabasi yameagizwa, inawezekana kati ya mwezi wa pili mpaka mwezi wa tatu yataanza kufika. Kwa njia ya Kimara - Mjini, sekta binafsi wataleta mabasi takriban 177 yanakuja kutoa huduma kwenye eneo hilo."

Ameongeza "Lakini pia sekta binafsi wameagiza Mabasi ya kutoka Mjini kwenda Mbagala takriban 755 ambayo yatakuja kutoa huduma kwenye eneo hilo, na mwezi wa tatu mambo yatakuwa sawa."

Pia soma ~ Desemba inaisha kimya, Makalla, Waziri Mchengerwa walituahidi Mwendokasi njia ya Mbagala zitakuwa zimeanza
 
Msemaji Mkuu wa Serikali, Gerson Msigwa, amesema mradi wa Mabasi yaendayo Kasi unatarajia kupokea Mabasi mapya kuanzia mwezi wa Pili hadi wa Tatu mwaka 2025

Akizungumza leo Januari 2, 2025 amesema "Tayari kuna Mabasi yameagizwa, inawezekana kati ya mwezi wa pili mpaka mwezi wa tatu yataanza kufika. Kwa njia ya Kimara - Mjini, sekta binafsi wataleta mabasi takriban 177 yanakuja kutoa huduma kwenye eneo hilo."

Ameongeza "Lakini pia sekta binafsi wameagiza Mabasi ya kutoka Mjini kwenda Mbagala takriban 755 ambayo yatakuja kutoa huduma kwenye eneo hilo, na mwezi wa tatu mambo yatakuwa sawa."
porojo tu. ...barabara yenyewe haipitiki sembuse mabasi ya BRT
 
Back
Top Bottom