Msema kweli mpenzi wa Mungu. Daraja la Kigamboni ndio lilinifanya kumpa kura yangu Dk. Magufuli

singidadodoma

JF-Expert Member
Nov 11, 2013
4,394
1,536
Ndugu wa Jf

Wakati wa uchaguzi kulikuwa na mchuano mkali baina ya Dk. Magufuli wa ccm na Lowassa wa Ukawa, siku moja nilitoka zangu huku Kwetu kiteto amabayo tangia uhuru ilikuwa haijawahi kupata lami lakini tulipata lami wakati Dk. Magufuli akiwa waziri wa miundombinu.
Nilipokuja Dar kwa safari ya kuwaona ndugu na jamaa nilitembelea Daraja la Kigamboni baada ya kuliona tu nikakakumbuka kuwa lilikuwa chini ya wizara ya Miundombinu amabayo ilikuwa chini ya Magufuli nikaona huyu ni mtu sahihi wa kupata kura yangu nikimlinganisha na Lowassa ambaye licha kuwa serikali zaidi miaka 30 lakini sijakiona cha maana alichosimamia na kukamilia.

Namshukuru Mungu sijapoteza kura yangu, ilikwenda kwa mtu sahihi,
AnC4Em4PgeBiOB7hi1Hlh8_-wDb8G7ZrnnwSr7k8k8-1.jpg

ArPfkvQU8oj6Ca4IRjzvncVXLcRB-oHsXvkcKL2-tB51.jpg

IMG-20160115-WA0015.jpg

IMG-20160115-WA0020.jpg

Imeelezwa kuwa daraja hili lililoanza kujengwa mwaka 2012 kwa Ushirikiano wa Mfuko wa NSSF na Kampuni za China, linatarajiwa kukamilika ujenzi wake mwaka huu. Daraja lina urefu wa mlalo wa kadirio la kilomita 2 likiunganisha Kurasini na Kigamboni.
 
Bado una tongotongo za Kibaya,Kiteto.
Unadhani wazo,design,funding,na implementation Ni ya Makufuli?
Think again
Bora umpe sifa Dr Ramadhan Dau
 
Watu hawajangudua kwamba kuvuka hilo daraja either kwa mguu au na chombo cha usafiri lazima ulipie. Na ndo maana wameweka hivyo vijumba kwa ajili ya kukatisha ticket. Kwa hiyo kigharama hamna unalolikwepa
 
mawazo mgando kuturudisha enzi za ujima..! Ujaze pantoni 6 au 7 kwa gati zipi?eneo lipi?umewaza meli zinazoingia bandarini zinapita wapi?Si ajabu wenye mawazo kama haya ni wale wale wanaopiga picha fly over 2 zilizopo Kenya na kuzirusha kuonyesha maendeleo..!!
 
Magufuli huwa anaongea kwa vitendo, yeye hufanya kitu kinachoonekana halafu anawaachia watu waanzishe mijadala miiingi. Hongera Ngosha, na bado yanakuja mambo meeeengi ya akili. Ukizingatia baraza lote la mawaziri ni madoctor na maprofesa.
 
Daraja imenifanya hata mm ninayeogopa panton nitakwenda kutembelea ndugu zangu kigamboni. Tumpe hongera Rais pale tunapoona panafaa.
 
Ni kweli kabisa hata MV Dsm ni matendo yake
Kuna jamaa pale Navy wanakaribia kugraduate kozi ya upakaji rangi wa vyombo vya majini. Watu wa Bagamoyo bado tunamkumbuka mheshimiwa alivyoipokea kwa mbwembwe hii makitu pale bandarini huku akituahidi kero ya mafoleni kwetu itakuwa historia. Badala ya kuwa historia sasa imekuwa makumbusho.
 
Ndugu wa Jf

Wakati wa uchaguzi kulikuwa na mchuano mkali baina ya Dk. Magufuli wa ccm na Lowassa wa Ukawa, siku moja nilitoka zangu huku Kwetu kiteto amabayo tangia uhuru ilikuwa haijawahi kupata lami lakini tulipata lami wakati Dk. Magufuli akiwa waziri wa miundombinu.
Nilipokuja Dar kwa safari ya kuwaona ndugu na jamaa nilitembelea Daraja la Kigamboni baada ya kuliona tu nikakakumbuka kuwa lilikuwa chini ya wizara ya Miundombinu amabayo ilikuwa chini ya Magufuli nikaona huyu ni mtu sahihi wa kupata kura yangu nikimlinganisha na Lowassa ambaye licha kuwa serikali zaidi miaka 30 lakini sijakiona cha maana alichosimamia na kukamilia.

Namshukuru Mungu sijapoteza kura yangu, ilikwenda kwa mtu sahihi,
AnC4Em4PgeBiOB7hi1Hlh8_-wDb8G7ZrnnwSr7k8k8-1.jpg

ArPfkvQU8oj6Ca4IRjzvncVXLcRB-oHsXvkcKL2-tB51.jpg

IMG-20160115-WA0015.jpg

IMG-20160115-WA0020.jpg

Imeelezwa kuwa daraja hili lililoanza kujengwa mwaka 2012 kwa Ushirikiano wa Mfuko wa NSSF na Kampuni za China, linatarajiwa kukamilika ujenzi wake mwaka huu. Daraja lina urefu wa mlalo wa kadirio la kilomita 2 likiunganisha Kurasini na Kigamboni.
Kama unataka ukuu wa Wilaya au Mkoa penyeza CV yako kwa Dr. JPM .
Kumsifia Hua haibadilishi msimamo wake....
 
Kila mradi nchini chini ya serekali ya majambazi hata uwe wa manufaa kwa wananchi ni deal wizi ufisadi wa kutisha na wa hali ya juu. Iyo billion 200 wameiba sana na Iyo ingetumika vizur madaraja mengine yangejengwa nchini kwenye vivuko.

Ni chama cha mashetan
 
Kila siku najiuliza hili
hili daraja na gharama zake....ni sawa?
bilioni zaidi ya 200 kuunganisha vitongoji vyenye wakazi chini ya laki tano?

Tungeweka pantoni za bilioni 7 tatu isingekidhi?

Nyani Ngabu Dark City Nguruvi3 ....
kwani hilo daraja ni kwa ajili ya wakazi wa kigamboni peke yao? hivi ile foleni kuanzia saa moja asubuhi pale feri kwenda kigamboni ni wakazi wa kigamboni wanarudi makwao asubuhi? hizo pantoni saba ungeorodhesha na ujenzi wa gati saba,baada ya miaka kadhaa tena uongeze nyingine saba. ushawahi kukaa ndani ya pantoni wakati mnasubiri meli ipite? mkuu hilo daraja litasaidia sana.
 
Back
Top Bottom