Msanii wa muziki Rehema Chalamila aka Ray C usiku wa jana alikamatwa na jeshi la polisi maeneo ya Kinondoni Manyanya almaarufu ‘Kinondoni kwa Mpemba’ jijini Dar es salaam baada ya kupiga makelele barabarani akidai anataka kutekwa.
Ray C akiwa kwenye gari la polisi
=================
More:
Hali ya kiafya ya mwanamuziki mkongwe Rehema Chalamila ‘Ray C, imeonesha kuwa tata kutokana na kile kinachodaiwa kuwa ni matumizi ya madawa ya kulevya jambo lililoleta sintofahamu baada ya video inayozunguka mitandaoni ikionyesha akichukuliwa na Polisi huku akisema kuwa wanamteka.
Habari zinadai kuwa mama yake mzazi amekuwa akikesha kumtafuta mrembo huyo kutokana na kuzama kwenye vijiwe vya mateja wa madawa hayo na kushindwa kuonekana nyumbani kwani kwa siku kadhaa na watu kujitokeza kumsaidia bila mafanikio.
Sambamba na hilo siku za hivi karibuni mwanamuziki Jay Dee, alionekana kuwa naye karibu na kudai kuwa Ray C, anahitaji marafiki wazuri na watu wavumilivu kuweza kumsaidia kwani kumlaumu pekee hakuwezi kumjenga bali ni kumzidi kumharibu kisaikolojia.
Mmoja wa wasanii wa Bongo Movie, Esha Buheti, kupitia mtandao wa kijamii ameweza kueleza jinsi gani alivyoguswa baada ya kumuoa Ray C akiwa chini ya ulinzi wa polisi akiwa hajitambui na kuongea maneno yasiyoeleweka na kudai kuwa awali alijua mrembo huyo anasingiziwa tuu.
Ameandika “Nashindwa hata niongee nini jamani, Ray C leo Kinondoni umenitoa machozi, jamani tufanye kitu tumsaidie Ray C, I mean it jamani siku zote nlikuwa najua anaonewa ila nilichokishuhudia leo nimeumia kutoka moyoni amedhalilika mwanamke mwenzetu, jamani tufanyeje?”
Akaendelea “Nilikua na Kabula, Kinondono kwa wapemba tumefuata chips mara tukasikia mtu anasema me Ray C nataka kuvua nguo, nikajua utani kushuka ni Ray C anasema nishikeni kuna watu wanataka kuniteka, alikuwa na nguvu sana watu kumshika akaanza kuongea vitu havieleweki, akaanza kutafuta kisu ajichome, watu walimzuia sana walishindwa akaanza kugaragara kwenye matope akipiga kelele,”
“Kiukweli nilijikuta nalia mara ikaja gari ya polisi ikambeba ila kwa tabu sana alikua akipiga kelele jamani nisaidieni msiniache kiukweli mpaka Ray C anaondoka na ile gari ya polisi sikujua anapelekwa wapi alikuwa kama mtu alopata kichaa, YARRAB TUNAMSAIDIAJE RAYC?”.