Nimemaliza form 4 mwaka 2015 mwaka huu nataka kujiunga na chuo sasa naomba mnishauri ndugu zangu nikasomee course gani ambayo yenye mafanikio pindi nikihitimu huko ngazi za mbele iwe diploma au labda mbele zaidi ila kwa sasa nahitaji kuanza na certificate sasa ipi au zipi course lukuki, sio afya because sikusoma science, so naomba msaada wenu NDUGU ZANGU
Huko tuendako Ajira inazidi kuwa ngumu.Jiunge au tafuta on job training ya ufundi wowote ule kwanza kwa mwaka mmoja halafu ujiunge na VETA kuongeza weledi na upate cheti baada ya hapo waweza jiajiri.Nakushauri jifunze umeme wa magari haya ya kisasa.