Msaada: Water pump haipandishi maji ila motor inazunguka

mgange hussein

Senior Member
Sep 10, 2012
159
43
Naomba msaada wenu wa mawazo.

Ninayo water pump zile zinazoingizwa ndani ya kisima cha maji.
Sasa tatizo lililopo motor yake inazunguka ila maji haipandishi inapandisha kidogo halafu inagoma ila motor inazunguka.

Sasa inaweza kuwa ni pump yake au capasita imekufa kabla sijachukua fundi akanitapeli.
Nitashukuru kwa mawazo
 
Kama ni pump ya kudumbukiza kwenye kisima maana yake, pump yako inatumia Impeller kuyachota maji, na kwa mzunguko wa motor maanayake ni kwamba, kadiri moto inavyo zunguka kwa kasi ndivyo wingi wa maji unavyo chotwa na kusukumwa kwenye juu.
Hivyo......
Ikiwa motor inazunguka, lakini maji hayapandi juu, au yanakua yamepunguza mwendo kasi...
Hapo yawezekana pump yaka inakabiliwa na matatizo yafuatayo.
1: Yawezekana pump imevuta matope
2: Yawezekana kuna mizizi, au taka ngumu zimenasa impeller
3: Yawezekana chujio (strainer) imezibwa na taka
4: Yawezekana vipande vya mawe vimeingia kwenye mfumo wa kunyonya maji
 
Na kama motor inazungusha impeller kwa kiunganishi cha coupling, basi yawezekana pia pakawa na tatizo la loose connection au misalignment kati ya motor, shaft, coupling, key, impeller.
Kama utaweza kuipiga picha, ebu fanya namna hiyo ili tukusaidie
 
Njoo nkuuzie kwa bei nafuu mkuu uachane na usumbufu huo tena fanya kabla ya kesho kutwa maana kuna muhindi mmoja anaitaka ila siwapend hao jama
 
Nunua Pump za Pedrollo toka Italy yako ni wap ??
Mkuu.....
Ebu acha kumdanganya huyu mleta uzi.
Pump zote za pedrollo, hazina uwezo wa kuvuta maji ya kina.
Pum hizi zimetengenezwa special kwaajili ya maji yanayo shukua kwa mgandamizo toka juu (gravity), na maji yanayo toka kwenye mlalo (zero degree).
Hizi pump zina zungushwa na motor inayo unganisha shaft kwa bush (spider), ambayo onaungana na couple inayo tokea kwenye impeller ya wima (Horizontal)
 
Are u sure?
 
Na kama motor inazungusha impeller kwa kiunganishi cha coupling, basi yawezekana pia pakawa na tatizo la loose connection au misalignment kati ya motor, shaft, coupling, key, impeller.
Kama utaweza kuipiga picha, ebu fanya namna hiyo ili tukusaidie
Safi kabisa mtalaam. Nilikuwa na tatizo kama hilo, nikanunua pump nyingine lakini tatizo likawa palepale. Nilileta fundi na katika kufanya uchunguzi wa tatizo akagundua nyaya zilizokuwa zikipeleka moto kwenye hiyo pump ndizo zilikuwa na matatizo na kusababisha motor isizunguke kwa kasi kubwa. Tulipobadili hizo waya mambo yakawa safi kabisa.
 
Are u sure?
1474867210199.jpg
1474867221346.jpg
1474867228014.jpg

Hizi ndio aina ya water pumps unazo mshauri mdau anunue.
Haya ebu tuambie hata moja ya hizo pum unaidumbikiza aje kisimani?
Nimesha kuambia uache uongo na lugha za ushawishi kwa kumpotisha mtu
 
Mbona Povu ungesema Pedrollo hakuna za kwenda chini mita 100 don't take things too Personal
Hakuna povu mkuu, hapa tunachambua mambo kitaalam.. .
Kinacho kupa shida ni kutochambua hizi mambo kitaalam, zaidi naona unaitangaza na kuisifia brandy.
Binafsi sina maslahi na kampuni yeyote, na wala sina mahusiano na yeyote muuza au mnunua pump ya maji.
Hapa huna elimishana tu.
Bilashaka nimekuwekea hata picha ya hizo pump unazo zisifia, haya tuelezee kitaalam inavutaje maji pasipo kukaririshwa kwamba unavuta umbali wa 100 meters....
 
Back
Top Bottom