Msaada wa usafiri kwenda Lindi

sulejman

Member
Jun 25, 2016
35
30
Habari za mchana.
Natumaini mko na afya njema.
Nahitaji kujua napata wapi usafiri (basi) wa kwenda Lindi kutokea Dar es Salaam, najua humu kuna watu wengi na wenye maarifa mengi hivyo nimeona niwashirikishe kwa faida yangu na wengine.

NB: Nikipata taarifa kampuni gani iko vizur na bei zake nitashukuru zaidi

Natanguliza shukrani.
 
Bus zipo nyingi tu nenda Temeke Sudan ndo ofisi za magari yanayoenda kusini zipo na kampuni zenye bus kali ni Hizi, Buti la Zungu, Baraka, Maning nice, Machinga.
 
Bei ilikua ni 23,000/= sijajua kwa sasa baada ya kupanda bei.

Weka maximum ya 27,000/=

Bus nzuri zipo nyingi
Buti la Zungu
Navil
Baraka Classic
King Yassin.
Tashrifu (Toka Tanga)
Manning Nice

Kama wewe una mahaba na mwendo basi subiri ile Tashrifu inayotoka Tanga, au Baraka Classic ya Kutoka Dodoma

Ila kama unapenda mwendo wa kawaida tu King Yasin, Buti la Zungu n.k
 
Back
Top Bottom