Msaada wa tafsiri ya ndoto hii

Misunderstood

JF-Expert Member
Aug 4, 2020
384
883
Habari za asubuhi!
Naombeni msaada wa tafsiri kwa ndoto hii niliyoota usiku wa kuamkia leo.

Nimeota nilivaa viatu, tukiwa kwenye kikundi tukaingia kama kwenye darasa au mkutano ingawa sikumbuki nini kilifanyika humo.

Muda wa kutoka natafuta viatu vyangu sivioni wakati wa kuzunguka kutafuta nakutana na mtu ananiambia vile ni viatu vyake na amevifua vikawa vimelowana tepe!

Nikabaki sina viatu vya kuvaa! Kikawaida inaonekana ni ndoto tu lakini kiroho nahisi ina maana sana ingawa nimejaribu kugoogle maana nilizozikuta hazinipa maana hasa.

Kama kuna mtu yoyote anayeweza kutafsiri ndoto tafadhali naomba msaada.
Asante
 
Ngoja akina Yusuf na Daniel watakuja kutupa maana yake Ila hata Mimi naona hiyo ndoto ina maana kubwa maishani mwako
 
Angalia sana mipango uliyonayo au ushauri unaopewa sio wako rudi kwa Mungu akupe mpango wake juu yako. Musa na Yoshua waliambiwa vua viatu vyako.. viatu ni decision
 
Mi sio mtaalam sana tena ila katika ulimwengu wa kiroho nyayo zako ni hatma ndo maana kuna verse kwnye bible nyayo zako kikikombolewa miguu yako itakuwa ya makomeo ya chuma na shaba yani ni nguvu ya kukombolewa maadui ndo mana kuna watu waliuana kisa kukanyaga mafuta(joking),hata huku uswazi watu hurogana kwa kuchotana unyayo Pia kumbuka kuwa tumepewa mamlaka ya kukanyaga ng'e na nyoka(yani maadui zetu)so nahisi kwa asilimia kubwa ndoto yako ni ya maono na inaashiria ushindi mkubwa dhidi ya maadui zako.Japo vita kama ni za kiroho huwa sio nyepesi wish you all the best.Ngoja wakali wa kazi waje maana ndoto ni ulimwengu mpana unaweza ukaota unapanda kumbe unashuka
 
Hapo mkuu kunauwezekano mkubwa WA kupewa mamlaka kuwaongoza wenzako ila utawaongoza kwa Muda mfupi sana na mamlaka hayo atapewa mtu mwingine .Bwana akubariki

Asee asante kwa ufafanuzi! Sasa nifanyaje? Maana kujua ni jambo la kwanza, cha kufanya je?
 
Mi sio mtaalam sana tena ila katika ulimwengu wa kiroho nyayo zako ni hatma ndo maana kuna verse kwnye bible nyayo zako kikikombolewa miguu yako itakuwa ya makomeo ya chuma na shaba yani ni nguvu ya kukombolewa maadui ndo mana kuna watu waliuana kisa kukanyaga mafuta(joking),hata huku uswazi watu hurogana kwa kuchotana unyayo Pia kumbuka kuwa tumepewa mamlaka ya kukanyaga ng'e na nyoka(yani maadui zetu)so nahisi kwa asilimia kubwa ndoto yako ni ya maono na inaashiria ushindi mkubwa dhidi ya maadui zako.Japo vita kama ni za kiroho huwa sio nyepesi wish you all the best.Ngoja wakali wa kazi waje maana ndoto ni ulimwengu mpana unaweza ukaota unapanda kumbe unashuka

Najua kaka! Yaani ndoto ni kitu kikubwa sana kiroho, maisha yanaweza kuharibika kupitia ndoto au hata kuwa mazuri! Ilimradi ujue maana na kitu cha kufanya. Ndoto si kitu cha kupuuzia kabisa
 
Ndoto yako ina maana kubwa kiroho

Ooh nimehisi hivyo! Ndomana nikaamua kuulizia zaidi na si kwamba siotagi ndoto zingine bali nimeona hii ina kitu ndomana nikaona nichukue hatua ya kuuliza maana, nahata kufanyia maombi ikiwezekana. Basi naomba niambie maana yake
 
Huyo aliyechukua viatu vyako ndotoni ni jiwe na ndoto inamaanisha mkimpa mitano mingine mtanyang'anywa hata kile kidogo mlicho nacho
#stay awake,
#beware of jiwe,
#beware of dreams,
#stay safe
 
Asee asante kwa ufafanuzi! Sasa nifanyaje? Maana kujua ni jambo la kwanza, cha kufanya je?
Kwanza Jambo la kwanza Kama imani yako sawa na Mimi, yaani mkristo, nyunyiza damu ya Yesu juu ya ndoto uliyoota, na ukatae maagano yoyote yaliyofanyika juu yako na nguvu za Giza,ninaamini utakuwa salama
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom