Msaada wa sheria ya ardhi

Mbimbinho

JF-Expert Member
Aug 1, 2009
8,328
7,783
Habari zenu wakuu.,

Ninaomba kujua sheria hapa ikoje, nielezee kwa kifupi tu swala lenyewe.

Mzee wangu mimi alinunua kiwanja maeneo ya kibaha, ni kiwanja kilichopimwa kabisa. Yeye aliuziwa kihalali kabisa kwa kuihusisha serikali ya mtaa ule na mtendaji akiwa mmoja wa viongozi waliokuwepo katika mauziano hayo.
Nyaraka zote halali za mauziano mzee wangu anazo.

Sasa tatizo limekuja baada ya aliyekuwa mke/mtalaka wa aliyeuza kiwanja kusema kuwa wakati wa talaka mahakama ilitoa uamuzi kuwa kiwanja kile kiuzwe then huyu mama apate asilimia kadhaa ya pesa ya mauzo., Mtalaka huyo anasema alimwambia aliyekuwa mme wake kuwa wasiuze ili kije baadaye kiwasaidie watoto na wakakubaliana hivyo mbele ya mahakama kuwa kama wameamua hivyo basi mahakama itabariki uamuzi wao.

Lakini baada ya miaka kadhaa huyu mme aliamua kukiuza kiwanja bila kumshirikisha mtalaka wake. Huyu mama mtalaka baada ya kupata taarifa akaja kushtaki kwenye serikali ya mtaa ambako mzee wangu akaitwa kwenye shauri hilo. Yule jamaa (mme mtalaka) aliyeuza kiwanja hapatikani na hajulikani anakoishi. Sasa kwa kuwa wamemkosa wamepitisha shauri kuwa mzee wangu ampe yule mama mtalikwa sh mil 1.75., na kama akishindwa watapiga mnada kiwanja alichonunua mzee. Mzee alinunua kiwanja mil 17.

Wakuu naomba kujua, kulingana na sheria je hawa jamaa wako sahihi? sheria inasemaje hapo maana mzee wangu alinunua kihalali na dokumenti zote muhimu anazo.
Msaada wakuu
 
Ardhi ni mali ya familia, hivyo unaponunua hakikisha mume, mke na watoto wanasaini, vinginevyo kugeukwa ni rahisi na kuanza masuala ya migogoro isiyokuwa na lazima.
Watakuja wajuzi zaidi wakushauri
 
We nazani azikutoshi sasa kama mmeambiwa mumlipe uyo mama milion 1.7 ili yaishe simumlipe kama mmenunua kiwanja m17 lipeni haraka mkienda mahakamani mtatumia zaidi ya iyo na ukumu itatolewa baada ya miaka
 
Mkuu asante, ingawa mimi nilitaka kujua hapo sheria inasemaje kama tumenunua kihalali na documents zote za serikali tunazo. After all aliyesema tumlipe huyo mama hiyo hela ni mwenyekiti wa mtaa sio mahakama.
 
Hawako

Hawako sawa. Hapo Mzee hahusiki na jambo hilo, Sheria huhitaji uwepo wa makubaliano ya wanandoa kabla ya kuuza Mali ya ndoa.

Kama nimekupata vema Mzee kanunua Ardhi baada ya talaka kwaio hakukua na ndoa.

Ardhi hio imenunuliwa kwa bei ya kwenye mkataba hio 1.7 ya nini tena? Kwa kuongeza baraza la Ardhi la kata katika maeneo ya nini ka kibaha hayana mamlaka kushulikia migogoro ya Ardhi.

Hakuna uwezekano wa hivo vitisho kuwa kweli.
 
Asante sana mkuu na nimekupata vyema. Kwa hiyo kwa case hii ambapo wakati wa talaka iliamriwa kiwanja kiuzwe then mwanamke apewe percent kadhaa ya mauzo, ila wakakubaliana kutokuiuza kwa ajili ya watoto. Lakini baadaye jamaa akaja kuiuza bila kumtaarifu mama (kutokana na maelezo ya huyu mama) Hapo hiyo ya jamaa kuuza bila kumtaarifu mtalaka wake inaweza kuwa na effect yoyote kwa mzee wangu??
 
Kina hati? Nani alishuhudia mauziano? Nani aliandika mkataba wa mauziano? Kwa jicho la awali sioni kama Mzee anahusika. Huyo muuzaji kama alikiuka makubaliano yao, wamtafute wao ili atoe gawio kwa mtalaka sio mnunuzi!
 
Documents zote muhimu za mauziano pamoja na ile barua toka katika serikali ya mtaa kuidhinisha kuwa mzee apewe hati mzee anazo, ndio alikuwa kwenye process ya mwisho kulipia ili apate hati yake.
Walioshuhudia mauziano ukiondoa mashahidi wa pande mbili, alikuwepo mtendaji wa mtaa pamoja na mwenyekiti wa mtaa.
 
M nachojua Ardhi yenye Thamani zaidi ya Mil 5 kesi yake huwa haiwezi kusikilizwa na Village land council.
Lakini vilevile Sheria ya Ardhi inamtaka mnunuaji kutafuta taarifa muhimu kuhusu kiwanja kutoka kwenye vyanzo muhimu kama ofc za Ardhi ili kujiridhisha kwamba Ardhi husika haina mgogoro kabla ya kununuliwa ucpofanya hvo unaweza poteza haki yako.
Ushauri wangu next tym mnapofanya manunuzi ya Ardhi kwa watu wenye au waliowahi kuwa na Familia hakikisha wanandoa wanaridhia na kama hawapo pamoja tafuta namna ya kujua ni kwa nn hawapo pamoja na kama walipeana taraka nn yalikuwa makubaliano ya taraka zile kama ilivo amuliwa na Mabaraza ya usuruhishi au Mahakama maana muda mwingine muuzaji hatokwambia kila ktu yy lengo lake itakuwa apate chake asepe yanayofuata unajijua mwenyewe.

Broh. M nakushauri mwambien Mzee wako kama ana hyo pesa ampatie huyo mama aokoe muda wa kusumbuliwa kwenda mahakani na kupoteza resources kuendesha kesi kwa ajili ya ktu kdogo kama hko, alichokitoa ni kikubwa kuliko kilichobaki. And kama ataamua hvo ahakikishe huyo mama anakusanya watoto wote ambao kimsimgi maamuzi yalitolewa kwa kuwa angalia wao huko Mahakani ili nao waridhie wasije wakasumbua baadae baada ya Baba Mama kubeba kilocho chao.
 
Huo ndio ukweli hizo ni moja ya mali za wanandoa waliozichuma pamoja haijalishi kipato cha mke ama mume mchango wa mke katika kiwanja hicho sio lazima kiwe pesa hata kukupigia masalo ya nyanya nyumbani na kukufulia jamhuri inatambua kuwa ni mchango wake. Mali zitathimiwa na kugaiwa kwa asilimia fulani saaa kama mume anauwezo wa kumlipa amlipa na sio mume hata mke akiwa nayo anampa mume mali inakuwa ya mtu mmoja mkiwa wote wavuja jasho kinauzwa mnagawana sheria kipindi hicho haikuwahi kufikiria maslai ya watoto maana wakati mnaoa hapakuwa na watoto
 
Wapo sahihi kabisa mkuu maana Mzee wako alishindwa kufanya reasonable inspection ili aweze kufahamu ukweli kuhusu hicho kiwanja kama kipo katika migogoro ya hapa na pale..kisheria hiyo inaitwa constructive notice.
 
Mkuu, sasa ikiwa hiki kiwanja kina hati halali kwa jina la muuzaji ni kitu gani Zaidi mnunuzi atafanya hiyo constructive notice ? mnunuzi wapi atakwenda kupata uhakika kuwa kiwanja kina uzika bila tatizo maana itakuwa shida kuanza kuzunguka na kuwauliza watu.
 
Mkuu ni kwamba mbali na kuoneshwa hati halali ya kiwanja buyer(mnunuaji) anatakiwa afanye utafiti katika hicho kiwanja kama nilivoelezea hapo juu na sehemu ya kufanya inspection ni katika office zinazohusiana na masula ya ardhi etc.
 
Mkuu ni kwamba mbali na kuoneshwa hati halali ya kiwanja buyer(mnunuaji) anatakiwa afanye utafiti katika hicho kiwanja kama nilivoelezea hapo juu na sehemu ya kufanya inspection ni katika office zinazohusiana na masula ya ardhi etc.
Wapo sahihi kabisa mkuu maana Mzee wako alishindwa kufanya reasonable inspection ili aweze kufahamu ukweli kuhusu hicho kiwanja kama kipo katika migogoro ya hapa na pale..kisheria hiyo inaitwa constructive notice.

Wakuu asanteni kwa michango yenu. Kuhusu kiwanja wakati wa kununua tulishirikisha upande wa serikali pia kitengo cha ardhi na hadi kubadilisha umiliki ulifanyika chini ya serikali kwa kuwa kiwanja hakikuwa na matatizo.
Wakati wa hukumu ya talaka yao, mahakama iliamua kuwa kiwanja kiuzwe then mwanamke apewa asilimia kadhaa, lakini yule mme wake mtalaka akasema wasiuze ili kiwe kwa ajili ya watoto. Lakini baada ya miaka kadhaa yule mwanaume akakiuka makubaliano waliowekeana na mkewe/mtalaka wake na kuamua kuuza bila kumshirikisha mke/mtalaka wake.

Siku ya mauziano muuzaji alikuja na mke wake mpya as a family na kwa kuwa hata mwenyekiti wa mtaa, afisa mtendaji walikuwepo mzee wangu akajiridhisha pasipokuwa na shaka kuwa kiwanja hakina tatizo na kuamua kununua mbele ya ushahidi wa serikali ya mtaa. Hiyo ilikuwa mwaka 2014.
Mwezi huu ndio huyo mtalaka anajitokeza. Wakuu hali ndivyo ilivyo, sasa hapo mzee wangu anakosa gani?? Au alitakiwa afanye nini kama mazingira yaliyokuwepo na yalipofanyika mauziano yalikuwa ni halali which makes the documents valid.
 
Mkuu asante, ingawa mimi nilitaka kujua hapo sheria inasemaje kama tumenunua kihalali na documents zote za serikali tunazo. After all aliyesema tumlipe huyo mama hiyo hela ni mwenyekiti wa mtaa sio mahakama.
Muone advocate achana JF humu kumevamiwa na wahuni hapana maana tena!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…