Msaada wa namna ya kuweka zuio la shambulio ( restraining order )

Andres

JF-Expert Member
Dec 4, 2013
501
799
Msaada wa kisheria unahitajika

Nina rafiki wa kike ambaye hapo mwanzo alikuwa na mahusiano na mwanaume ambaye walikuja kuachana kutokana na tabia za jamaa kutompendeza mwanamke.

Hapo kabla Waliishi pamoja ingawa hawakuwa na ndoa rasmi, na katika kipindi hicho walijaaliwa mtoto mmoja.

Sasa shida inakuja baada ya huyu rafiki yangu kuachana na yule jamaa, jamaa ameshindwa kabisa kumove on bali ana mharass huyu msichana consistently. Ni kwamba huyu binti akianza mahusiano na mtu mwingine, basi jamaa atakuja kuanzisha fujo, anamfanyia huyu binti full stocking, na anajitambulisha kwa watu anasema ni mke wangu sema tumegombana tu, hapa nipo napambania ndoa yangu.

Sasa hii hali inamtesa sana huyu rafiki yangu, for real anaona yupo kifungoni, naombeni ninyi wajuvi wa sheria zetu za kitanzania mnipe muongozo ni kitu gani nimshauri cha kisheria anachoweza kufanya ili aondokane na kadhia hii.
 
Wazo zuri, changamoto niliona wanasema Tz restraining order kisheria ni for the property tu
 
Ampeleke polisi ajieleze kila kitu, huyo bwana ataitwa atajieleza na yeye, binti ataulizwa kama bado anampenda bwana akisema HAPANA, polisi atamgeukia bwana na kumwambia "Mwanamke akishasema Hapana hakuna Mtu yoyote atakayesema Ndio, kwa hiyo Kijana vumilia maumivu kwa muda utazoea na utamsahau"

Wataandikishwa wote wawili incase Bwana katoa vitisho, fujo au chochote cha uvunjifu wa Amani basi Binti apeleke malalamiko haraka na hatua kali za kisheria zitachukuliwa, na Bwana ataonywa kukaa mbali na huyo Binti,

Baadaa ya hapo watapelekwa Dawati la Jinsia ambapo watapewa maelekezo jinsi ya kumtunza Mtoto, na Bwana ataandika maelezo ya kujifunga ili akienda kinyume sheria kali imshukie,

Kila Mtu ataondoka nyumbani kwake Mmoja akiwa na Hasira na Maumivu na mwengine akiwa na Amani na Furaha.

NB: Baada ya hapo huyo Binti asimuongeleshe bwana maneno ya nyodo awe mpole lakini asiwe zoba sababu Watu wa hivyo mwisho wao hua kudhuru, hawana la kupoteza.
 
Thank you dear
 
Njoo nikulinde .........mi huyo jamaa yako akizingua nampaka futa la mwamposa mchana kweupe...usije Tu kumuonea huruma
 
Wewe jamaa umeoa Mke wa MTU kienyeji enyeji tu pasipo kufuata procedures, na mbaya zaidi unajikosha kwa kujipa tumaini kuwa hawakuwa na ndoa rasmi hivi-sijui kwako wewe unadhani ndoa rasmi ni IPI hiyo ya kuishi pamoja tayari ni rasmi na Mahakama inatambua.

Kuna Dada Dream queen kakushauri hapo,lakini haya mambo ya ndoa kiafrica afrika unabidi uwende beyond maana inaweza kushinda huko Polisi na Mahakama -jamaa akaamua kufuata upande wa pili wa shilingi a.k.a ndumba wote mkakosa.

Mie nakushauri kabla hujaanza kutatua tatizo hilo kiserikali,anza kifamilia mtafute suluhu kwa kuhusisha familia yako,ya binti na ya huyo jamaa muyamalize lasivyo unacheza kifo mkononi.Kumbuka kwenye Mapenzi& Hela mwanadamu anaweza fanya lolote baya hata kama ni mdogo kama piriton au fukara.
 
Sasa mwanangu unanilinda jamaa yangu kivipi ? Unazingua boy
 
Ushauri mzuri though umejaribu kuwa nabii au sheikh yahya kwa kutengeneza scenario ambayo haipo hivyo.. mimi sijaoa huyu binti, she is muu friend kama nilivyoeleza chief. Ingekua mke au something of the sort ningekuwa nishalivalia njuga mwenyewe
 
Hatari sana, kama unamla mle sana mpaka akafungue shauri mahakamani Kwa hiari yake, wanawake usiwaamini sana. Dawa ni kula mzigo Kwa kishindo
 
Msaada wa kisheria unahitajika

Nina rafiki wa kike ambaye hapo mwanzo alikuwa na mahusiano na mwanaume ambaye walikuja kuachana kutokana na tabia za jamaa kutompendeza mwanamke.

Hapo kabla Waliishi pamoja ingawa hawakuwa na ndoa rasmi, na katika kipindi hicho walijaaliwa mtoto mmoja.

Sasa shida inakuja baada ya huyu rafiki yangu kuachana na yule jamaa, jamaa ameshindwa kabisa kumove on bali ana mharass huyu msichana consistently. Ni kwamba huyu binti akianza mahusiano na mtu mwingine, basi jamaa atakuja kuanzisha fujo, anamfanyia huyu binti full stocking, na anajitambulisha kwa watu anasema ni mke wangu sema tumegombana tu, hapa nipo napambania ndoa yangu.

Sasa hii hali inamtesa sana huyu rafiki yangu, for real anaona yupo kifungoni, naombeni ninyi wajuvi wa sheria zetu za kitanzania mnipe muongozo ni kitu gani nimshauri cha kisheria anachoweza kufanya ili aondokane na kadhia hii.
Naomba kabla sijachangia niruhusu nikurekebishe matumizi sahihi ya maneno

Hapo ulipoweka neno Consistently ilitakiwa kukaa neno Constantly. Naomba urekebishe.

Hapo ulipoweka neno stocking ilitakiwa likae nano Stalking.

Haya maneno kimatamshi yanasound the same ila yanamatumizi tofauti .
 
Kwa maoni yangu nashauri huyu rafiki yako amekurupuka sana kuanzisha mahusiano mapya huku akiwa bado yupo katika complicated relationship na huyu baba mtoto wake.

Hili ni jambo muhimu sana kuzingatia unapoanza uhusiano na binti, ni vema sana kujua alipotoka kimahusiano na alimalizana vipi na mtu aliyekuwa uhusiano wa mwisho.

Kuna mtu anamuacha mwenzake kimya kimya bila mazungumzo, majadiliano wala kumalizana kokote yaani akili za kitoto kabisa.

Matokeo yake anaanzisha mahusiano na mtu mpya ambaye anaingia na kukutana na mifarakano isiyo na mbele wala nyuma ambayo inavuruga hata amani ya uhusiano mpya.

Huyo ni mtu ambaye amepata nae mtoto. Anaweza kuwa ni mkorofi au wameshindwana ila alitakiwa wakae chini na watu wazima kisha wayamalize na kukubaliana juu ya malezi ya mtoto na namna watashirikiana.

Hizi ndio shida za kuvutana magetoni na kunyanduana kizembe kisha ujauzito juu mnaaza kuvurugana baadae sababu hamkwenda kiutaratibu na kwa kufuata misingi na taratibu zinazotakiwa kijamii kuishi pamoja.

Mwambie rafiki yako kabla hajaenda polisi akumbuke huyo anaekwenda mchukulia restraining order ni baba wa mtoto wake.

Pengine huyo mwanaume bado anamhitaji na sababu anamfanyia fujo ni hofu ya kutojua yeye, rafiki yako na mwanae wanakwenda wapi na kuishi na nani. Ni vema akamtafuta akiwa na wazee wakae wayazungumze na aeleweshwe ili yasijekutokea mengine.

Na nyie watoto wa kike siku hizi mna mambo ya kibwege sana kulala na mtu hujui hata familia na historia yake ipoje. Wengine ni vichaa wa akili huwa vinalala tu na kuibuka kipindi fulani fulani.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom