Mr George Francis
JF-Expert Member
- Jun 27, 2022
- 234
- 366
MSAADA WA MWANADAMU UNA KIKOMO
Je, kuna msaada wa milele?
-Ni kweli tumesaidiwa sana na watu na tunaendelea kusaidiwa. Ni kweli pia tumewasaidia sana watu na tunaendelea kuwasaidia. Lakini pamoja na hayo yote tunapaswa kutambua kuwa msaada wa mwanadamu una kikomo chake.
-Hakuna binadamu yoyote atakayetusaidia milele na hata wale tunaowasaidia hatutawasaidia milele. Itafika wakati msaada huo utafika kikomo. "Hakuna msaada wa milele."
Lengo la kusema hivi ni nini?
-Lengo ni kutaka kutaka kusema kwamba unaposaidiwa na mtu katika jambo fulani unatakiwa ujijengee uwezo wa kujitegemea mweyewe pasipo msaada wa huyo anayekusaidia. Hii itakusaidia kujiondoa katika utumwa wa kuendelea kumtegemea mwanadamu. "Msaada ni utumwa uliojificha."
-Lakini pia hata wewe unayemsaidia mtu, kweli saidia kwa moyo lakini ruhusu mtu huyo akue kupitia wewe, ruhusu mtu huyo afanikiwe kupitia wewe. Usimuache tu akienenda katika njia zisizofaa ili baadae akishindwa uje kumsema eti "Nilimsaidia sana lakini mwenyewe alishindwa kujiongeza." Najua Hii kauli wengi mnaipenda sana. Achana na huo ubinafsi.
Je, ufanye nini?
-wewe unayesaidiwa kubali kujifunza, boresha kile unachojifunza mwisho wa siku tengeneza kitu chako kitakachokufanya usimame mwenyewe. Kusema "Ahsante" na kwenda kuanza maisha yako kwa amani halitakuwa kosa.
-wewe unayetoa msaada, kunjua moyo na toa nafasi bila choyo. Kama kuna support ya ushauri au fedha itahitajika toa tu with no expectations of return. "Mkono unaotoa ndio unaopokea." Mwenyezi Mungu aonae mpaka ndani ya moyo wako atakupa tuzo yako.
Je, waungwana hufanya nini?
-Linapokuja swala la kuachana mala baada ya kusaidiana kwa muda fulani, hapo ndipo ambapo malanyingi matatizo yanapoibuka. Mala maneno, mala ugomvi mala sijui nini. Yaani inshort hapa mambo huwa ni mengi lakini waungwana hatufanyi hivi.
-Muungwana anaachana na mtu kwa amani. Mtoa msaada na mpokea msaada wote wanakubaliana kuachana kwa amani na ikitokea kuhitajiana kwenye jambo moja na lingine hapo baadae vilevile busara hutumika kuwakutanisha pamoja.
Tatizo lipo wapi?
-Malanyingi tatizo huwa lipo kwa watu wa pembeni au wapambe. Hawa wana maneno mengi, hatakama busara ilifanyika baina ya wahusika wenyewe watu watazusha maneno mengi ya karaha ili ionekane kulikuwa na tatizo pahala.
- Msiwasikilize wala wasiwatoe kwenye mstari wa amani. Upendo uzidi kudumu kati yenu, kwasababu hata kama sio leo basi ingekuwa kesho. "Msaada wa milele haupo kwa mwanadamu bali ni Mungu pekee anayeweza kuwa pamoja na wewe siku zote."
Mwisho, usiweke tumaini kubwa sana kwa mwanadamu, weka tumaini lako lote kwa Mungu. Binadamu wanabadilika na wanaweza kukushangaza kwenye nyakati ambazo ungewahitaji zaidi.
Nakutakia kila lenye heri katika maisha yako. Mwenyezi Mungu akubariki sana. 🙏
It's me
A Lawyer and LifeCoach
Mr George Francis
mr.georgefrancis21@gmail.com