Msaada: Usumbufu wa Makampuni/Mitandao inayokopesha mtandaoni na nini cha kufanya

ndege joni

JF-Expert Member
May 23, 2017
679
1,101
Habari za mapumziko wote mtkaopata nafasi ya kusoma hii thread

Mada yangu inahusu makampuni au mitandao inayotoa mikopo online, ambayo wengi kwa namna moja ama nyingine wameweza kupata usumbufu. Sio lazima uwe umeshakopa hata pia matangazo yao unapojaribu kuingia kwenye Mitandao mingine.

Naweza kuweka katika makundi mawili
1. Usumbufu kabla ya kukopa
MAra nyingi ni matangazo yao mtandaoni, mfano YouTube na Mitandao mingine. Hii hukera sana kwanza inakula bundle zetu na kuchelewesha sana kuingia, kuna sometimes inahesabu muda ili uweze kukata.
Nahitaji kujua naweza kufanyaje ili niweze kuepuka matangazo hayo?
2. Usumbufu baada ya kukopa mtandaoni
Hapa ndio mtihani ulipo, kwa waliowahi kukopa mnanielewa vizuri. Hawa majamaa ni wasumbufu sana katika kudai, mara wanatisha kuwa wamepeleka jina kwenye taasisi zinazohusika na wadaiwa sugu, simu kila saa yani ni tabu tupu. Kumbuka wana riba kubwa, sijui wana vibali kutoka BOT ama la. Lakini ni moja ya mikopo kausha damu, kwa sababu unakopa na ndani ya muda mfupi (wengi ni wiki 1) unatakiwa kurudisha hela na riba zao.

N.B Wengi wanaojaribu kukopa ni wenye vipato vya kawaida, Wasiwasi usiokuwa na utafiti ni kwamba hawa majamaa wanatumia ushirikina (chuma ulete) kwa sababu pindi unapojihusisha kukopa hata kama kwa kujaribu pesa huanza kuwa ngumu sana na mambo kufeli. Ukiunganisha dots kwamba masharti ya mikopo yao ni nafuu, namba ya NIDA tu bila dhamana wala mdhamini yeyote. Hawakujui huwajui, hapa kuna kitu.
Nahitaji tu msaada kwamba nawezaje kuzuia matangazo yao kwenye simu yangu? Yamekuwa kero sana, pia serikali inawezaje kusaidia kwenye kudhibiti hizi kausha damu za mitandaoni? Najua kuna kitu inanufaika lakini kwa hawa nahisi kuna wizi mkubwa sana, kwa sababu unakopa kwa riba kubwa sana mf Tsh 20,0000 urudishe 26,000 kwa wiki ni wizi mkubwa sana
 
Mkuu ingependeza zaidi utaje hizo apps nione ambayo sijaikopa nivute pesa

Sinaga wasi na pesa zinazojileta namna hii, ukipiga simu napokea sio usumbufu kwangu mbele ya pesa

Wakipigiwa watu WA karibu sina chakupoteza maana naishia nao poa
 
Mkuu ingependeza zaidi utaje hizo apps nione ambayo sijaikopa nivute pesa

Sinaga wasi na pesa zinazojileta namna hii, ukipiga simu napokea sio usumbufu kwangu mbele ya pesa

Wakipigiwa watu WA karibu sina chakupoteza maana naishia nao poa
Mbona zipo nyingi sana mie nishapiga karibia kila kampuni nikaamua kutulia ila kero ni matangazo yao kwenye simu yangu
 
Hoja namba moja usitumie "YouTube" ya Bure tumia "premium" kwani hayo matangazo yanayokulia wewe bundle ndo yanakuwezesha wewe kupata hudumu Bure

Hoja ya pili ni acha kukopa au ukikopa lipa kwa wakati
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…