Msaada/ushauri: Nasikia sauti ya wadudu wanapekecha kwenye mbao darini ndani ya nyumba yangu

Wamuyaya

Member
Apr 4, 2021
72
69
Habari za kazi wadau!

Nina nyumba yangu ambayo nimeahamia mwaka jana, ingawa bado sijamalizia finishing. Mara baada ya kuhamia kwenye nyumba yangu nilishangazwa na kushtuswa na sauti za wadadu, ambazo baada ya kufanya uchunguzi nikagundua wanasikika ndani ya baadhi ya mbao darini.

Nyumba yangu bado sijaweka gypsum ingawa tayari nimeshafanya blandaring. Hii hali inaniogopesha hata kuweka gypsum wakati bado wadudu wanasikika wakipekecha kwenye baadhi ya mbao. Sauti za hawa wadudu zinakera sana hata kunikosesha usingizi.

Naombeni ushauri kupitia uzoefu wenu namna ya kukabiliana na hili tatizo. Natanguliza shukurani!
 
Dawa inaitwa Twiga Gama? Niweke sawa mkuu tafadhali!
Hiyo Dawa Nilishauriwa Na Fundi Mmoja Ingawa Sijui Kama Utaipata Inauzwa Kwenye Maduka Ya Vifaa Vya Ujenzi
Huwa Inapulizwa Kwenye Ceiling Board Ndani Ni Hatari Hiyo

Kuna Choo Cha Shimo Tuliimwaga Ndani Oops!! Iliuwa Mende Wengi Sana Kwa Muda Mfupi Yaani Wadudu Wakivuta Harufu Wanatoka Nduki Na Kufia Mbele
 
Dawa inaitwa Twiga Gama? Niweke sawa mkuu tafadhali!
Hii dawa imepigwa marufuku inapatikana kwa Magendo, mimi niliipata pele mwenge kwenye maduka ya hardware inauzwa tsh 45,000 ilinisaidia kidogo naendelea kusikilizia kama wataisha ingawa sijawaaikia sana
 
Kwenye Choo Cha Shimo Nilipoimwaga Iliuwa Mende Wengi Wanaojaa Ndoo Ndogo Ya Litres 10,Hatari Yaani Hiyo Hakisalii Kidudu Ndani
 
Hiyo Dawa Nilishauriwa Na Fundi Mmoja Ingawa Sijui Kama Utaipata Inauzwa Kwenye Maduka Ya Vifaa Vya Ujenzi
Huwa Inapulizwa Kwenye Ceiling Board Ndani Ni Hatari Hiyo

Kuna Choo Cha Shimo Tuliimwaga Ndani Oops!! Iliuwa Mende Wengi Sana Kwa Muda Mfupi Yaani Wadudu Wakivuta Harufu Wanatoka Nduki Na Kufia Mbele
Vipi Mchwa je? Inawaua pia
 
Back
Top Bottom