Msaada uonevu makazini

raisi2020

Member
Mar 4, 2016
82
83
Naomba sana msaada wa ushauri wa kumpa huyu mtu,kijana mmoja anaitwa jina X aliajiriwa kama mhudumu katika taasisi flan ya govt,alimaaliza masomo yake ya chuo na kupata proffessional(ujuzi) mwaka 2011.

Sasa toka amalize masomo yake alijitahidi kuomba kubadilishwa cheo katika taasisi hiyo lakini alikuwa anazungushwa kwa kusema kuwa wanarekebisha scheme of service,mwaka 2014 wakambadilisha kazi toka uhudumu kwenda fani aliyosomea kwa barua hii ni baada ya kuwa anasumbua kuomba kazi sana tena sana,muda wote huo akawa amesota na cheo cha uhudumu toka 2011-2014.

Akawa anaserve cheo kipya ila kwa mshahara ule ule wa uhudumu kwa sababu zile zile za scheme uku wakisema ikikaa sawa tutakupa mshahara wako unaostahiri,hivyo toka 2014 mpaka sasa 2017 anakamshahara hako hako ka uhudumu.

Je wadau huyu mtu tunaweza mpa ushauri gani mana hata promosheni za cheo chake cha uhudumu muda unapita abadiliki mshahara muda unakwenda umri unaenda.
 
Avumilie tu hamna namna manyanyaso ya kazi sio kwa x tu unless amepata kazi nyingine
 
Aache uoga siku moja amwendee afisa mwajiri amweleze ukweli wa maisha.Natamani nivae uhusika wake nimvae mwajiri au kiongozi wa juu yake.Hii dunia tu,ukiwa mwoga utasota sana,mimi huwa simwabudu mtu dunia hii ingawa sivunji sheria wala simtukani mtu yeyote
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…