Msaada: Ujauzito wa wiki 41 na hakuna uchungu

ZamdaIssa

JF-Expert Member
Nov 10, 2015
879
1,458
Jamani msaada!

Nina ndugu yangu ni mjamzito wa mtoto wake wa pili Kwasasa una muda wa wiki 41 ndio imeanza.

Mimba yake ya kwanza alijifungua kawaida katika wiki ya 37 salama kabisa!sasa ujauzito huu wa pili umemsumbua saaana mpaka leo hii hajajifungua na hakuna dalili.

Tarehe ya makadilio kwenye kadi iliandikwa tarehe 17/07 na baada ya Ultrasound ilisoma atajifungua tarehe 27/07 ila mpaka leo bado bilabila! Mama amechoka saana. Hospitali wamemwambia asubiri mpaka tarehe 29/7 ndipo arudi tena watajua cha kufanya!!

Msaada kwa aliyepitia changamoto hii alifanyaje.

UPDATES;Jamani ashukuriwe maulana,mama alijifungua salama August 06 kwa njia ya kawaida,mama na mtoto wote wako salama

Ahsanteni wote kwa ushauri,mawazo na muda wenu,mubarikiwe sana
 
Pole sana nakushauri uende hospitali kwa Mkunga wako au daktari kwa maelezo zaidi au subiria hiyo tarehe 29 urudi hospitali maana ndio wanajua taarifa zote
 
Ukute ana Cord mtoto hashukii...!! Hospital gani hiyo wanamwambia azidi kusubiri??? Poleni sana
 
Poleni kwa changamoto. Alienda hospital zinazoeleweka au ni hizi za uchochoroni? Kuweni makini kwani wajawazito wengi wanafariki kwa sababu ya maamuzi potofu ya wakunga na dr. Jaribuni kupata ushauri sehemu nyingine. BTW kwa nini wasimzalishe tu?
 
kikawaida mimba mwisho ni wiki 42 halaf hata hizo tarehe za ultra sound hazijafika na kikawaida mwanamke mjamzito hujifungua kuanzia wiki ya 36 mpaka 42 kama amepiga ultra sound na mtoto ameonekana yuko vyema asubiri hizo tarehe zifike aene hospital watamuanzishia uchungu
 
Mpaka wiki ya 42?....mbona mbali sana
 
Mpaka wiki ya 42?....mbona mbali sana
yeah japo ni wachache hufika huko, s unajua hua mimba inahesabiwa kwa wiki na sio mwezi mana kila wiki kunakua na mabadiliko kwamtoto wengine hujifungua kuanzia wiki 36, wiki 38, wiki 40 na had hukoo wiki42 yan ikifika hio 42 uchungu haujaanza automatic watakuanzishia tu
 
Poleni kwa changamoto. Alienda hospital zinazoeleweka au ni hizi za uchochoroni? Kuweni makini kwani wajawazito wengi wanafariki kwa sababu ya maamuzi potofu ya wakunga na dr. Jaribuni kupata ushauri sehemu nyingine. BTW kwa nini wasimzalishe tu?

Hospital alioenda ni Lugalo jeshini dar!ndio ameambiwa hivyo
 
Pole sana nakushauri uende hospitali kwa Mkunga wako au daktari kwa maelezo zaidi au subiria hiyo tarehe 29 urudi hospitali maana ndio wanajua taarifa zote

Ahsante mkuu tulienda ndio tukaambiwa hivyo!sasa mama amepata taharuki kubwa
 
kikawaida mimba mwisho ni wiki 42 halaf hata hizo tarehe za ultra sound hazijafika na kikawaida mwanamke mjamzito hujifungua kuanzia wiki ya 36 mpaka 42 kama amepiga ultra sound na mtoto ameonekana yuko vyema asubiri hizo tarehe zifike aene hospital watamuanzishia uchungu

Ahsante kwa Faraja mpenzi
 
Back
Top Bottom