MSAADA TUTANI: Ninaomba msaada namna ya ku-apply Songea Teachers' College

Nukes

Member
Jun 29, 2023
16
27
NB: Mada husika ipo kwenye paragraph ya pili.

Heshima kwa wanajukwaa wote, baada ya salamu naomba niende moja kwa moja kwenye jambo la msingi.

Mimi ni mhitimu wa kidato cha sita mwaka 2022 na ninahitaji kujiunga na chuo cha Ualimu cha Songea (Songea Teachers' College) ili nisomee Diploma kwa miaka miwili katika kozi ya Ualimu.

Nimejaribu kutafuta mtandaoni namna ya ku-apply lakini nakutana na subpage ambayo imekuwa attached kwenye website ya songea (kama sijakosea ni ya mkoa) ambayo haina link maalumu ya ku-apply chuo kwa muhula 2023/2024.

Kiufupi ni kwamba juhudi zangu zimegonga mwamba, ninaomba msaada wa maelezo kwa mtu yoyote ambaye atakuwa na ufahamu wa namna ya ku-apply.

Natanguliza shukrani zangu za dhati kwenu.
 
NB: Mada husika ipo kwenye paragraph ya pili.

Heshima kwa wanajukwaa wote, baada ya salamu naomba niende moja kwa moja kwenye jambo la msingi.

Mimi ni mhitimu wa kidato cha sita mwaka 2022 na ninahitaji kujiunga na chuo cha Ualimu cha Songea (Songea Teachers' College) ili nisomee special Diploma kwa miaka miwili katika kozi ya Ualimu.

Nimejaribu kutafuta mtandaoni namna ya ku-apply lakini nakutana na subpage ambayo imekuwa attached kwenye website ya songea (kama sijakosea ni ya mkoa) ambayo haina link maalumu ya ku-apply chuo kwa muhula 2023/2024.

Kiufupi ni kwamba juhudi zangu zimegonga mwamba, ninaomba msaada wa maelezo kwa mtu yoyote ambaye atakuwa na ufahamu wa namna ya ku-apply.

Natanguliza shukrani zangu za dhati kwenu.
Deadline ni leo,
Link ya kuapply: MOE | TCM

Maelezo :
 
Attachments

  • UALIMU.pdf
    316.2 KB · Views: 19
Pole mdogo wetu, Ulifanikiwa?
Hapana, nimepata taarifa kwamba dirisha la application za diploma za miaka miwili (kwa entry ya cheti cha kidato cha sita) hufanyika baada ya matokeo ya kidato cha sita ya mwaka husika (kwa case hii ni 2023/2024) kutolewa. Kwakuwa matokeo bado hata dirisha la application bado halijafunguliwa.
 
Back
Top Bottom