Msaada tutani: 2grfse (Crown Athlete), inalia knock kwa mbali sometime hailii kabisa na iko fresh, engine power haipungui.

chilubi

JF-Expert Member
Sep 21, 2011
8,187
6,244
Habari wadau,
Nimekwama hapa, mana hakuna check engine light inayowaka.
Gari inalia knock kwa mbali lakini nikiwa naendesha, huwa inapotea, ila nikisimama naanza kusikia mlio wa knock. Saa nyengine nikiwa idle, hakuna mlio wa knock kabisa, engine inanguruma vizuri tu, na sometime ikiwa idle, inaweza ikaja ikisha ikaondoka inajirudia ivo mpaka itanyamaza na kuwa normal kabisa.

Sasa nimeona nianze na spark, nimezitoa, nikazipiga msasa (lengo ni kujua kama ni detonation nockk au mechanical knock)nikazirudisha, ikapotea moja kwa moja, nimeendesha gari kama wiki ivi under normal driving, haikurudi. ila leo nikasema niikanyage, ebana wee, kusimama tu ile knock ikaja tena, halafu ikapotea. nikazitoa plug nikazipiga tena msasa (najua haitakiwi kuzipiga msasa lakini ndio diagnosis ya chini ya muembe kwanza) ikatulia, nikaendesha kama 15km normal driving, ishu imerudi tena ikafanya kulia kama mara 2 au 3 ivi ikakata. Nikasema isiwe tabu, nikatia plug mpya, ikawa kimya baada ya mda inalia tena.

ingekuwa knock ya kwamba labda piston aur bearing imeenda zake, basi mlio ungekuwa unaendelea kila nikiendesha, lakini huu mlio mara unaondoka na mara unarudi. Na nina uhakika unatokea kwenye engine maana nimetega sikio vizuri.

Note: Haiwaki check engine na engine sijaona iki loose power. Mlio unatoka juu kwenye mashine.
Engine ni 2grfse.
 
Cha kwanza hapo nunua plug Og funga kwa hatua ya kwanza, maana kwa maelezo yako hapo hapo haihusiani na main na corn, maana main na corn ikilia hulia moja kwa moja
 
Kwa maelezo yako kitu ninachokifikiria ni valve lifter(s). Modern cars mostly zinakuwa equiped na hydraulic valve lifters ambapo zikianza kufail (kujamm) zinaweza kuleta mlio wa knock kwa wakati na mara nyingi ni ikiwa idle.
Inabidi kufuatilia zaidi mfumo wa hizo engine nipate uhakika. Na utengenezaji wake ni kwenye cylinder head tu asikuambie mtu ubomoe engine yote. So ukiwa na new timing belt/chain kit, head gasket na hizo valve lifters mpya you are good to go.
 
Ila kwa maelezo ya mtoa mada anasema kuwa akisafisha Spark Plug hiyo shida inapotea kwa muda
 
Huo mchezo umenikuta sana kwenye 4GR Athlete. Nikaamua niuze bei ya hasara tu. Now nipo na 3GR Athlete nakula maisha tu.
hizi GR engine zina matatizo yenye kufanana mana mfumo ndio ule ule tofauti ni engine capacity ndio imetofautiana. Sasa bro hukuihangaika 4gr? mana angalau nikapata idea kile ulichofanya
 
Cha kwanza hapo nunua plug Og funga kwa hatua ya kwanza, maana kwa maelezo yako hapo hapo haihusiani na main na corn, maana main na corn ikilia hulia moja kwa moja
Nimenunua brand new plugs, lakini sio za denso wala NGK. halafu huu mlio unatoka sehemu hio hio, kama sio cylinder 5 basi ni 3 (upande wa dereva) pale kenye maeneo ya ile d4 pump. kwa sababu upande wa abiria ni kawaida tu. sasa pia nawaza isijekuwa hii high fuel pressure pump nayo pia inazingua, mana kuna siku niliwasha engine nikaisikia ina whine, engine ikawaka kisha ikazima apo apo, nikajaribu tena engine ikawaka, lakini hii ilitokea one time tu haikutokea tena.

Kinachinikera ni kuwa check engine light haiwaki. angalau ningejua wapi pa kuanzia.
 
Mimi inaniudhi mkwaruzo fulani nikiwasha gari mara kwanza asubuhi. Kama engine haina oil vile. Au timing chain sijajua solution yake.
Hiyo ni oil pump tu mkuu. Ila ukibadilisha sio mbaya ukaweka na timing chain nyingine.
 
hizi GR engine zina matatizo yenye kufanana mana mfumo ndio ule ule tofauti ni engine capacity ndio imetofautiana. Sasa bro hukuihangaika 4gr? mana angalau nikapata idea kile ulichofanya
Hamna mkuu, sikuhangaika nayo kabisa.
 
Check engine inawaka kwa issues zinazoaffect emissions mkuu. Sheria za kulinda mazingira za huko majuu zimeainisha hilo. Mfumo wa uchomaji wa mafuta na usafishwaji wa moshi ukiwa na shida ndio check engine itawaka.

Hivyo mechanical knock haitaweza kukuletea check engine. Hata detonation knock ya sensor inaweza isiwashe check engine pia. Itabidi uchomeke diagnosis machine uangalie yaliyomo.

Huenda unapofanya hizo services za plug na kuwasha gari kisha linatulia kwa dakika kadhaa, sio kwasababu umetibu tatizo bali ni kwasababu gari imepoa.

Kuna uhusiano gani kati ya mlio na joto la engine?

Umejaribu kutumia oil nzito kidogo kuliko specification ya gari ili kuona kama inakaa kimya?
 
Knock inaweza kusababishwa na matatizo makubwa zaidi kama vile piston slap, worn bearings, au matatizo kwenye cylinder head. Tafuta fundi apige service ya maana
 
Check engine inawaka kwa issues zinazoaffect emissions mkuu. Sheria za kulinda mazingira za huko majuu zimeainisha hilo. Mfumo wa uchomaji wa mafuta na usafishwaji wa moshi ukiwa na shida ndio check engine itawaka.

Hivyo mechanical knock haitaweza kukuletea check engine. Hata detonation knock ya sensor inaweza isiwashe check engine pia. Itabidi uchomeke diagnosis machine uangalie yaliyomo.

Huenda unapofanya hizo services za plug na kuwasha gari kisha linatulia kwa dakika kadhaa, sio kwasababu umetibu tatizo bali ni kwasababu gari imepoa.

Kuna uhusiano gani kati ya mlio na joto la engine?

Umejaribu kutumia oil nzito kidogo kuliko specification ya gari ili kuona kama inakaa kimya?
Hakuna uhusiano kati ya mlio na joto la engine. huu mlio hautokei ikiwa nita drive kikawaida. Ila nikianza kukanyaga mafuta mfano na overtake au hata kama nakanyaga tu kwa nguvu basi nikimaliza kukanyaga ndio mlio unakuja.

Sijatia oil ilokuwa nzito, naweka recommended engine oil ya 5w30.

Finally, after a very long drive, na kwa siku kadhaa kuiendesha, gari imewaka check engine, imekuja na P0012, P0014 na P0017 kwa pamoja. nimetoa battery, nimerudisha na kuendesha hadi lreo code hazijatokea tena, lakini mlio unakuja.

P0012 - Camshaft A Position Timing - Over retarded Bank 1
P0014 - Camshaft B Position timing Over Advanced bank 1
P0017 - Crankshaft Position Camshaft Position Corelation (Bank 1 Sensor B)
 
Weka diagnosis mashine kubwa mkuu huenda kuna codes zimekuwa set ila hazijawasha MIL (check engine)

Kuhusu mlio unahitaji sikio la fundi mechanic, akiskia atang'amua ni nini.

Anzia kwa autoelectrician mzuri mmoja yupo humu then atakups recommendation za kwenda mechanical
 
Back
Top Bottom