MSAADA: Tatizo ni meno kuwa na rangi nyeusi (Meno 🦷)

Father of Chemistry

JF-Expert Member
May 21, 2021
401
1,282
HABARINI ZA WEEKEND WANA JF,

Natumai mu buheri wa afya.

Kwa Ufupi Mimi ni kijana wa kiume miaka 22. Ni mwanafunzi wa chuo kikuu kimojawapo apa Tanzania.

Nimeandika huu uzi kuomba msaada ni dawa gani nzuri ya meno au tiba ambayo itatumika kungarisha meno. Apa tatizo ni meno kuwa na rangi nyeusi kwa upande wa ndani na hata kwa baadhi ya meno unajitokeza kwa upande wa nje.

Hata inakuwa vigumu kucheka au kutabasamu mbele ya watu. Nimetumia dawa za meno kama Colgate ila zinaondoka unjano lakini huo weusi weusi hauondoki.

Naamini hili jukwaa lina wataalamu au muhanga aliyeikimbia hii shida. Ndio maana naamini nitapata suluhisho la hili tatizo.

Na pia hili tatizo liko kwa watu wengi sana. Naamini ushauri wenu utakuwa msaada kwa watu wengi.

Nawasilisha.
 
Mimi sio mtaalamu wa kinywa ila huwa naona meno yakianza weusi yana dalili ya kuoza jitahidi uwe unapiga mswaki asubuhi na jioni ili usiwe una lala na mabaki ya chakula mdomoni.
 
Dah Mimi meno yangu, yanatoboka tu yanakua meusi lakini hayaumi, napiga mswaki asubuhi na jioni...sasahivi jino la mbele limeanza kutoboka kutoboka lakini hayaumi
 
Nenda kwa dentist ukasafishe, kimsingi binadamu wote kwa mwaka tunatakiwa kuchech afya ya kinywa angalau mara mbili kwa mwaka.

Ile sehemu imeandikwa Dentist wabongo tunajuwa ni kwa ajili ya wanaokwenda kung'oa meno tu.
 
Fata huu ushauri mzuri sana, lakini pia weusi kweny meno unaeza ukawa pia unasababishwa na utumiaj wa kahawa, sigara etc, cha msing nenda hospital kwa ajili ya checkup na usafishwe kwa kutumia vifaa maalum huo weusi utaisha
 
Hapo Regency Hospital wana huduma ya kusafisha meno, uwe na bima inafaa zaidi.

Sukutua twice a day pia ni muhimu.

Ukiweza tumia mswaki wa mti then changanya dawa unayotumia na majivu kidogo

Natumia hii hapa 👇
 
Attachments

  • 20220813_080837.jpg
    20220813_080837.jpg
    137.3 KB · Views: 45
HABARINI ZA WEEKEND WANA JF,

Natumai mu buheri wa afya.

Kwa Ufupi Mimi ni kijana wa kiume miaka 22. Ni mwanafunzi wa chuo kikuu kimojawapo apa Tanzania.

Nimeandika huu uzi kuomba msaada ni dawa gani nzuri ya meno au tiba ambayo itatumika kungarisha meno. Apa tatizo ni meno kuwa na rangi nyeusi kwa upande wa ndani na hata kwa baadhi ya meno unajitokeza kwa upande wa nje.

Hata inakuwa vigumu kucheka au kutabasamu mbele ya watu. Nimetumia dawa za meno kama Colgate ila zinaondoka unjano lakini huo weusi weusi hauondoki.

Naamini hili jukwaa lina wataalamu au muhanga aliyeikimbia hii shida. Ndio maana naamini nitapata suluhisho la hili tatizo.

Na pia hili tatizo liko kwa watu wengi sana. Naamini ushauri wenu utakuwa msaada kwa watu wengi.

Nawasilisha.
Me nahisi hayo ndio maumbile yako na hakuna aibu Kama umeumbwa hivyo hata ukaimuwa kufanya tiba bado ttzo lotarudi tu
Really me naweza maliza week 1 au zaid bila kupiga mswaki na meno bado yako safi wala kinywa hakitoi harufu coz sijapata lalamiko lolotekwa wafu so piga mwaki tu inatosha mungu kukuumba hivyo labda ndio uzima wa meno yako
 
Uchafu huo mkuu usisapot ndo unaondoka kwa teeth scaling and polishing.
 
Hapo Regency Hospital wana huduma ya kusafisha meno, uwe na bima inafaa zaidi.

Sukutua twice a day pia ni muhimu.

Ukiweza tumia mswaki wa mti then changanya dawa unayotumia na majivu kidogo

Natumia hii hapa 👇
Hii hospital ya Regency iko wapi madam kwa Dar ?, naomba unielekeze !
 
Back
Top Bottom