Msaada: Tatizo la mimba kutoka kutokana na Presha

Mangi flani hivi

JF-Expert Member
Jan 2, 2016
2,026
3,104
Mdau anaomba msaada toka kwa wajuzi wa hili tatizo:

Mke wake amekuwa akipata tatizo la mimba kuharibika kwa kutokana na presha. Kila akifikisha miezi6 hali inabadilika na mwishoe mtoto hufia tumboni. Ameshawaconsult magainae Kama wawili hivi, lakini bado hawatoi suluhisho la tatizo moja kwa moja. Wanamanage presha ikifika Miezi tajwa Hali inabadilika. Tafwadhali mwenye wazo juu ya hili atusaidie.

Naomba kuwasilisha.
 
Mke wake amekuwa akipata tatizo la mimba kuharibika kwa kutokana na presha. Kila akifikisha miezi6 hali inabadilika na mwishoe mtoto hufia tumboni
nadhan maelezo mazuri wangetoa hao unawaita magainae " obstreticians and gynecologists", kwa mtazamo wangu maelezo yako hayatoshi kabisa kwa mtu humu jf kutoa suluhisho sahihi. nafikiri ni vema ungetaja umri wa huyo mmwanamke, zimeharibika mimba ngapi?, na je umri wa mimba kuharibika unaongezeka au unapungua? na je dalili zipi za awali kabla ya mimba kuharibika, historia ya huyo mwanamke pia?

nmejiuliza pia kuhusu hao magainae 'madaktari bingwa wa magonjwa ya kina mama'
1.kwamba je wamefanya vipimo vingine kujiridhisha siyo pressure tu inayosababisha ujauzito kuharibika? na je hata kama ni pressure wamejiridhisha haina primary cause? kifafa cha mimba je?
2. je kama kweli ni pressure, wana manage vipi pressure kwa mama mjamzito? je wapo sahihi
3. kiutaratibu daktari kitu kikimshinda ana fanya refarral kwa wakuu wake au hospitali ya juu zaidi..

ushauri
aombe maelezo ya kina kwa hao hao magaina, awaombe na barua ya referral aende hospitali ya juu zaidi.
 
Pole Sana
Huku Kuna Watu Wanaweza Kukusaidia
CC : MziziMkavu
 
Pole; dada yangu alipoteza mtoto. Mtoto alifia tumbon

Dr alimshaur atoe mimba sababu presha inasababisha kifafa cha mimba pia na aliambiwa angeweza zaa mtoto ambaye si mkamilifu kiakil.

Lakin sasa hv ana mtoto; tulimwomba Mungu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…