Msaada tafsiri ya hii ndoto

JT wa Dommy

Member
Sep 15, 2016
29
38
Habari wapendwa. Nimekuwa nikiota hizi ndoto za nyoka mfululizo nashindwa kuelewa kwanini.
Juzi niliota niko kwenye nyumba imezingirwa na nyoka wa aina tofauti wengine hata sijawahi kuwaona wa ajabuajabu wapo kwenye kila chumba isipokuwa chumba tulichokuwepo sisi (nilikuwa na watu wengine kama 5) wakati tunajiuliza tufanyeje nikaamka.
Leo nimeota wakati nazunguuka nyuma ya nyumba yetu kukagua kagua (nyumba yenyewe haifanani na ya kwetu kiuhalisia) nimedumbukia kwenye kisima kidogo kilichojaa nyoka wadogowadogo wengi sana ila kwa bahati nzuri nikajivuta juu nikatoka. Nilishtuka nikaamka ila baada ya muda kidogo nikalala tena nikaota kuna linyoka likubwa sana halafu mweusi sana kuna watu wanapambana nalo, mimi lakini nimesimama kwa mbali naangalia, kwenye hao watu wanaohangaika kumdhibiti huyo nyoka kuna msichana ambaye yupo na mbwa wake bahati mbaya yule nyoka akamng'ata mbwa. watu wa pembeni yangu wakawa wanasema huyo mbwa hawezi pona maana yule nyoka ni black mamba akikuuma unakufa hapohapo. Na ni kweli sekunde chache tu mbwa akafa. Na mimi nikaamka

Sasa jamani sielewi hizi ndoto zinamaanisha nini kwa kweli ningekuwa nimeangalia kipindi cha wanyama au movie ya kutisha au chochote kuhusu nyoka sawa ila sijawahi hivi karibuni.

Wenye kujua tasfiri nisaidieni mwenzenu.
 
mshana ukuje huku utoe msaada ila pole sana jitahidi kusali sana
 
Pole sana..jiweke karibu na mungu.. Nyoka ni tafsiri ya uwepo wa maadui
 
Unalindwa na nguvu ya MUNGU but Majaribu na shetani yapo karibu yako you have to be humble infront of GOD otherwise ndugu yangu utakumbwa na Majaribu mazito sana
 
Dah.......Labda maruweruwe ya uhakiki wa vyeti tu....usijali yameishapita
 
Pole mkuu iliwah na mimi kunitokea hiyo kitu nikawa nasari sana nakukemea ndoto mbovu, za kutisha ikapotea hiyo hari Hivo MUNGU NI MWEMA ALIYENISHINDIA MIMI NAWE ATAKUSHINDIA.. KABLA YA KULALA SAlI SANA.
 
Unalindwa na nguvu ya MUNGU but Majaribu na shetani yapo karibu yako you have to be humble infront of GOD otherwise ndugu yangu utakumbwa na Majaribu mazito sana
Asante sana mdau. Ni kweli nilijisahau sana kwenye kusali nashukuru sasa nitarudi kwenye mstari
 
Pole mkuu iliwah na mimi kunitokea hiyo kitu nikawa nasari sana nakukemea ndoto mbovu, za kutisha ikapotea hiyo hari Hivo MUNGU NI MWEMA ALIYENISHINDIA MIMI NAWE ATAKUSHINDIA.. KABLA YA KULALA SARI SANA.
Asante mkuu. Binadamu huwa tunajisahau sana haswa kwenye sala sasa narudi kwenye mstari ni Kusali kwa kwenda mbele
 

Similar Discussions

Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…