Msaada: Nina tatizo la maskio kuunguruma kwa muda mrefu

Wapendwa

Nina tatizo la maskio kuunguruma kwa muda mrefu.

Msaada wa mtu anaejua matibabu
Pole sana.

Unatakiwa uonane na daktari bingwa wa masikio, pua na koo (ENT surgeon) ili akuchunguze na kukupima masikio yako ili kubaini tatizo linalokusumbua na hatimaye upatiwe matibabu sahihi.

Kila lakheri.
 
Wapendwa

Nina tatizo la maskio kuunguruma kwa muda mrefu.

Msaada wa mtu anaejua matibabu
Ungejieleza vizuri sikio linanguruma vipi, binafsi nishawahi kupata tatizo kama hilo sema mimi nilikuwa nasikia "siiiiiiiiiiiiiiiiiiii" endelevu na isiokuwa namwisho, mchana unaisikia kwa mbali ila ikifika usiku au ukiwa mahali tulivu basi sauti inakuwa kali zaidi

Haina dawa ila unatakiwa kujifunza kuishi nayo, mimi nilijifunza kuizoea na nilikaa miezi ikaja kupetea yenyewe bila hata kujua hapa wewe ulivyoandika hivi ndio na mimi nimekumbuka

Nadhani niliipata baada ya maji kuingia masikioni na kupelekea sikio kuuma kwa muda mrefu bila matibabu
 
Ok, sawa!

Nafikiri ni vyema akaenda hospital kuonana na wataalamu wa masikio, ni vigumu sana kujua kama tatizo lako na lake yanafanana. Pia nafikiri sio sahihi kusema moja kwa moja kwamba hali hiyo haina dawa. Kuna watu wanapata matatizo ya kiafya na huchelewa kwenda kutafuta huduma hospital kwa sababu walishauriwa kwamba hakuna tiba wakati vipimo na tiba vipo. Muhimu aende hospital tatizo libainike na kama tiba ipo atapata tu.
 
Ubarikiwe sana na Mungu akubariki
 
Pole ndugu MUNGU akuponye na kukusaidia je umepata msaada tayari
 
Ndy ilionekana Sina shida yoyote ya mfumo ndan ya sikio ila madaktar walisem hio Hela wakat mwingine Haina chanzo maalumu kwaio yanipasa kuizoea
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom