MSAADA: Nasumbuliwa na miguu kuuma, hasa mguu wa kushoto

Uhuru24

JF-Expert Member
May 2, 2015
4,053
4,297
Nasumbuliwa na miguu kuuma hasa wa kushoto, hivi karibuni nikasogea kwenye zahanati wakaniambia kwamba huo mguu hauumi isipokuwa una ganzi.

Basi wakanifungashia dawa fulani hivi za NATB, ila mguu unauma sana kwenye vidole pindi unapotembea.

Yaani kuanzia kwenye vidole hadi kwenye vigimbi wakati wa kutembea napata shida haswa.

Hivyo basi mwenye kujua, kufahamu wapi naweza pata tiba au nini cha kufanya waweza share nami.

Asanteni.
 
Pamoja na yote upande wa mama husumbuliwa na matatizo haya ya miguu.
Mimi mguu unachoma kwenye nyayo,harafu ili utembee basi yakupasa vidole uvifinye kwa chini ndio upate balance y kutembea.
Nako kwenye unyayo kama kuna chomachoma
 
Unakuwaje mkuu
Kunakuwa na tatizo la Mizimu au Uchawi..

Mguu ni hatua zako..

Mguu unapouma inaonyesha kuwa Kuna kifungo Cha hatua yaani kusonga mbele kimaendeleo...

NB: Hii sio kwa kila mguu unapouma basi ni upande wa mama, ni mguu unapouma bila kuumia yaani bila kuwa na shida yeyote kiafya.
 
Kama ni ganzi halafu wanaufunga tena? Si ndo wanazuiya hata damu kufika kwenye mishipa ?

Kama una mafuta ya upako 😎 paka nunua na dawa inaitwa salmia upake.

Usiufunge uache wazi.

Achana na soda and sugar.

Pole
 
Kunakuwa na tatizo la Mizimu au Uchawi..

Mguu ni hatua zako..

Mguu unapouma inaonyesha kuwa Kuna kifungo Cha hatua yaani kusonga mbele kimaendeleo...

NB: Hii sio kwa kila mguu unapouma basi ni upande wa mama, ni mguu unapouma bila kuumia yaani bila kuwa na shida yeyote kiafya.
Sijaumia,sivuti sigara,sinywi pombe ila ni tatizo ambalo lilitokea basi nikawa nadharau sasa naona limefika pagumu.Nameza dawa leo siku ya 39 maana kila siku nameza kidonge kimoja ila bado.
 
Hapana siufungi,ila unachoma kwenye unyayo na hayo mafuta unasema wewe ya upako mtu kanipa wala hakuna jipya
 
Babu yangu alisumbuliwa na mguu kwa miaka mingi sana. Akienda hospital hapewi majibu ya kueleweka.

Mwezi wa saba aliwekwa mguu kwenye beseni akatoka funza. Wazungu wakachukua vipimo KCMC bahati mbaya vikapotea, wakachukua vingine wakatuma Ocean Road.

Tukiwa tunasubiria majibu tarehe 8 mwezi oktoba, akafariki tarehe 3. Alikuwa akiwa na maumivu makali sana. Miaka miwili kabla ya kifo ilikuwa ni kulia na kuomboleza so sad.

Usipuuze maumivu tafuta tiba kwa gharama yeyote na mawazo ya kitaalamu
 
Sijaumia,sivuti sigara,sinywi pombe ila ni tatizo ambalo lilitokea basi nikawa nadharau sasa naona limefika pagumu.Nameza dawa leo siku ya 39 maana kila siku nameza kidonge kimoja ila bado.
Huwezi ona ni tatizo, sababu unakuwa hujaumia hivyo unajipa moyo utapona...

Hii hali wengi hawaijui inatesa wengi..
 
Nasumbuliwa na miguu kuuma hasa wa kushoto, hivi karibuni nikasogea kwenye zahanati wakaniambia kwamba huo mguu hauumi isipokuwa una ganzi.

Basi wakanifungashia dawa fulani hivi za NATB, ila mguu unauma sana kwenye vidole pindi unapotembea.

Yaani kuanzia kwenye vidole hadi kwenye vigimbi wakati wa kutembea napata shida haswa.

Hivyo basi mwenye kujua, kufahamu wapi naweza pata tiba au nini cha kufanya waweza share nami.

Asanteni.
Pamoja na kutafuta matibabu, fanya yafuatayo:
1. Acha kabisa kunywa vinywaji vyenye sukari kama vile juice, soda na bia laini
2. Acha kula wali, ugali, mikate
3. Kula vyakula vya protini kwa wingi, huko huko utapata carbohydrates za kwenye ugali na wali.
4. Kula mboga mboga
 
Babu yangu alisumbuliwa na mguu kwa miaka mingi sana. Akienda hospital hapewi majibu ya kueleweka.

Mwezi wa saba aliwekwa mguu kwenye beseni akatoka funza. Wazungu wakachukua vipimo KCMC bahati mbaya vikapotea, wakachukua vingine wakatuma Ocean Road.

Tukiwa tunasubiria majibu tarehe 8 mwezi oktoba, akafariki tarehe 3. Alikuwa akiwa na maumivu makali sana. Miaka miwili kabla ya kifo ilikuwa ni kulia na kuomboleza so sad.

Usipuuze maumivu tafuta tiba kwa gharama yeyote na mawazo ya kitaalamu
Mguu wa kulia ni upande wa baba...

Hata uende Ulaya kutibiwa huwezi pona Wala kuona tatizo maana hayo ni mambo ya nguvu za giza...

Tatizo Huwa halionekani...
 
Hilo ni tatizo la mishipa ya fahamu.
Nenda kwenye hosipitali kubwa zenye wataalam wa fani hiyo utatibiwa na utapona kabisa.

Pole sana!
Shukrani mkuu hebu nidokezee hospital hata moja nipo daslam
 
Back
Top Bottom