Msaada : Mwenye kuelewa juu ya kutambua EFD receipt fake

kijana wa leo

JF-Expert Member
Nov 28, 2011
2,921
7,173
Habarini wakuu,

Kulingana na kasi ya serilkali ya awamu ya 5 wananchi wengi tumekua na mwamko wa kulipa kodi hasa pale tunapofanya manunuzi makubwa na madogo. Kwa faida ya wengi yeyote mwenye uelewa juu ya hizi receipt za EFD (E-Fiscal Devises) atusaidie namna ya kutofautisha receipt fake na original.Mara nyingi ukienda kufanya manunuzi hasa maduka ya posta na kkoo unaambiwa bei mbili tofauti (Bei kubwa na ndogo) na zote unapewa electronic receipt ya yenye thamani ya kile ulicholipia ila ya bei ndogo unaambiwa ni fake.
Najua kuna hata ambao hatuambiwi unapewa tu receipt unajua umechangia pato la taifa kumbe wajanja wanapiga.
Karibuni tuchangie ili tusiojua tujue.
 
Unanunua tairi nne, jamaa wanaandika moja kiujanja ujanja
Tusipo elimishana nchi yetu haiwezi kuendelea sa ivi atleast serikali inaonesha matumaini, inabidi tuiunge mkono kwa kuhakikisha tuna changia pato la taifa kadri tuwezavyo.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…