Nifanye Nini Nataka Kumuoa Lakini Bado Anawasiliana Na X Wake?
Ntamani kujua zaidi hasa kusikia kwa wanawake, mimi ni kijana wa miaka 32 sijaoa ila nina mpenzi wangu ambaye niko naye kwenye mahusiano kwa miaka minne sasa. Wakati nakutana na huyu Dada alikua ametoka kwenye ndoa yake, mwanaume wake alikua ni mtu wa kumnyanyasa sana.
Alikua na wanawake wengi na mara nyingi alikua ni kumpiga mpaka kumfungia ndani. Ndugu zake walishaongea sana kuhusiana na kumuacha huyo mwanaume lakini kila akirudishwa nyumbani anakaa kidogo anarudi kwa mwanaume wake, si kwamba kuna alichokua akikipata, hapana ni utaje tu wa mateso.
Baada ya muda yeye mwenyewe kuna kipindi alichoka, ilifikia hatua huyo mwanaume alimpiga sana akashindwa kuvumilia, alichukua kisu na kutaka kumchoma huyo mwanaume na hapo ndipo ulikua mwisho wao, aliondoka yeye mwenyewe ingawa mwanaume aliomba msamaha san alakini hakurudi.
Wakati nakutana naye walikua na kama miaka miwili wameachana kwa talaka kabisa. Nilimpenda na nilitaka kuingia naye kwenye mahusiano lakini ilikua shida sana kwake kupenda upya. Ana watoto wawili ambao alizaa na mume wake na ni miaka 6 sasa mwanaume hajawahi hata kupiga simu kuulizia wanae kwani kahamia kwa mwanamke mwingine ambaye anamlea na hataki hao watoto.
Nilihangaika sana kumpata huyu dada, kwanza alikua haamini kuwa anaweza kupendwa na wanae wawili na pili alikua bado hana kazi ya kueleweka. Kwakua nilimpenda nilianza na wanae, nilikua nao karibu nikawaopenda wakanipenda kama Baba, nilipowaonyesha wanae upendo ndipo alianza kuniamini na tukaanza mahusiano.
Niseme tu ilikua ngumu sana kuwa naye kwenye mahusiano, si kwakua alikua bado anamkumbuka X wake bali kila kitu nilichokua nakifanya alikua haamini. Yaani ni kama haamini kuwa nampenda, ana wasiwasi sana na kuona kama namchezea, nilimfungulia Biashara na kumfanyia vitu vingi sana lakini kila sakika ananiuliza kwanini namfanyia hivyo.
Klwanini nimpende wakati yeye ana watoto wawili? Kwanini nawapenda wanae hivi tukija kuzaa wakwetu si nitawachukia wakweke? Anakua na wasiwasi kiasi kwamba kuna wakati namuelewa ila naboreka kwani anaweza kukasirtika kwa kitua mbacho hata hujui kama umjefanya na baadaye akija kukuambia unashangaa hivi mimi hapa kosa lango liko wapi?
Kwa mfano, sikui moja nilimtoa out, tukaenda sehemu imechangamka, sasa kule kulikua na wadada wamevaa kihasarahasara na wazuri tu, sikuhangaika nao ni kama uko zako kariakoo kila mtu anapita, alininunia wiki nzima hayuko sawa anaongea tu kwa mafumbo kuja kumuuliza ananiambia bora tuachane?
Nilishangaa mpaka nikaanza kujihisi labda nimechapuka, alikua anakazania kuachana nikaanza kukagua na simu yangu labda hata shetani alinitumia meseji ya mapenzi ili kunigombanisha lakini wapi? Kumuuliza sana ndiyo aliniambia kwanini nilimpeleka kwenye hoteli ambayo ina wadada wazuri ni kama nilienda kumringishie niende nikawaoe wao?
Kusema kweli nilishindwa kama nakasirika au nafanya nini? Kwamaana nilimpeleka hoteli kubwa kwaajmili ya kula maisha, kule kuna watu wengi wanakuja na mambo yao, siwezi kukaa mlangoni kukagua na kusema wasiingie na vimini, yaani nilishangaa, hilo si tukio moja, nikuwa kwenye mitandao nishid ahata ukilike picha bahati mbaya atafutilia na kusema unataka kumuacha.
Nampenda sana na nimekubali kuwa kwakua aliumizwa sana basi kuna vitu nitapaswa kumuelewa na kuzidi kumuonyesha upendo wa kweli. Lakini sababu yangu mpaka kukutafuta ni hivi, nataka kuoa, nataka kumuoa lakini yeye anasema hayuko tayari kwa ndoa kwasasa, kila mtu anamshangaa kwani nimefanya kila kitu lakini anasema hataki kuolewa tena.
Nikimuuliza shida ni nini ananiambia kuwa naweza kumuacha? Nimehangaika kwa tangu mwezi wa kwanza ili akubali hata nimvalishe pete lakini aligoma akaniambia nimpe muda. Nilipokazana sana aliniambia tuachane, akakataa nisiwaone wanae, hapokei simu zangu na kila mtu akimtafuta anamblock.
Kinachoniuma zaidi nikuwa, ndugu zangu wanataka sana nioe na wanajua niko naye, sasa baada ya kuniblock na kugoma kabisa, ndugu zake kuongea naye bila mafanikio Mama yangu alimpigia simu kwani nilishamtambulisha basi sijui waliongea nini lakini alimjibu vibaya wakagombana sana mpaka Mama akaniambia huyo si mwanamke wakuoa.
Mimi najua ni kwanini alifanya hivyo na bado nampenda lakini sasa hivi ndugu zangu hawaelewi wananiambia kama nikuoa basi nitaoa mimi mwenyewe hawamtaki. Mimi hilo si shida, shida nikuwa yeye akawa hataki kuwasiliana na mimi. Baada ya kuona na hataki kabisa mimi kuwaona watoto ambao ni kama wangu.
Wiki iliyopita nami nilichoka, nilichoamua ni kwenda kwa wazazi wake na kuwaambia kuwa nimeamua kujitoa hivyo yuko huru na maisha yake kwani mimi alikua hataki hata kuongea na mimi. Baada ya kufanya hivyo na kuona kwamba niko siriasi alinitafuta yeye na kuniomba msamaha akiniambia kuwa alikua haamini kuwa nampenda ndiyo maana alifanya hivyo.
Kwakua nampenda niliamua kumsamehe, ingaw abado nilikua sijaongea na ndugu zangu ila sikujali. Sina kawaida ya kushika simu yake lakini jana nikiwa chumbani nimekaa mara meseji ikaingia na ikaonekana pale juu.
“Achana na mume wangu, wewe is unaolewa tuache tuwe na amani.” Nilishtuka nikaichukua simu, nikaingia na kuanza kuikagua. Hapo ndipo nilipo9oona kuwa tangu mwezi wa kwanza kipindi nataka kwenda kwao kumbe X wake alijua kua nataka kumuoa. Alimtafuta na kuanza kumuomba samahani akimuambia antaka akurudi kwani kule ile ndoa yao na huyo mwanamke hawajapata mtoto.
Alimuambia asikubali kuolewa na mimi kwakua walipeata talaka moja tu hivyo bado anampenda na hataki matabaka ya watoto. Niliangalia meseji zao walizokua wanatumiana tangu kipindi hicho mwanamke anakataa lakini mwanaume anasisitiza anampenda. Kipindi alichokataa nisiwaone wanae walishawapeleka wka Baba yao na hakutaka niwaone kwakua wangeniambia.
Mwanaume alikua analalamika watoto wananipenda mimi na alikua anaomba ampe muda ili kumuacha mke wake. Alikua ananichelewesha ili kupima kama yule mwanaume atamuacha mke wake au la kwani alimuambia kabisa ili amkubali basi amuache mke wake.
Mpaka sasa hivi badon hawajaelewana, nimeona meseji na sijui chakufanya namuuliza hanipi jibu ananiambia nifanye maamuzi mwenyewe, nimechanganyikiwa hata sijui nifanye nini?