Msaada: Maeneo ya Maktaba (Libraries) ninayoweza kwenda kujisomea hapa Dar ukiondoa Maktaba Kuu ya Taifa

mzeemzima

Senior Member
Apr 14, 2010
122
78
Wadau,

Ukiondoa Maktaba Kuu ya Taifa, naomba kujuzwa kama kuna maktaba yeyote nyingine ambayo mtu yeyote anaweza akaenda kujisomea.

Naomba kama unajua jina, location, utaratibu, gharama ya maktaba na uwepo wa huduma za ziada kama umeme, internet, nk, katika maktaba hiyo au hizo pia utufahamishe.

Natanguliza shukrani.
 
Kuna ile ipo upande wa zile kasino mbili maarufu enzi hizo Califonia na Joly ni ya ubalozi (nimeusahu jina) ilikuwa bure na vitu unavyohitaji vipo tena bure.Wajuzi watakujuza zaidi.
 
Kila kitu siku hizi ni 'online' tu; unajifungia ndani unapakua vitabu uwezavyo na kuvimeza; ingia pdfdrive
 
Hivi kweli kuna watu bado wanawaza kwenda maktaba kusoma vitabu?

Vitabu vipo online bila idadi tena vingi ni BURE, hutaki vitabu pitia blogs kuna milions of blogs out there bado niende maktaba nifungue kitabu nisome?
 
Siyo wote wanao penda kusoma soft copy. Kuna wanao penda hard copy mkuu.
Ukijumlisha na mazingira wanao ishi unakuta hapajatulia tofauti na unapo enda library.
 
Back
Top Bottom