Msaada kwa wataalam wa Sound production

donlucchese

JF-Expert Member
Mar 23, 2011
17,123
21,871
Salam wakuu,

Straight to the point,naomba msaada kwa wataalam wa Sound engineering na production, Niko maeneo ya bunazi mkoa wa kagera na baada ya utafiti wa kina nikagndua kwamba kuna changamoto kubwa ya studio za wasanii kurekodia kazi zao.

Hivyo naomba ushauri wa kitaalamu je ni computer ya aina gani na yenye soundcard ipi itafaa, mic, mixer and everything needed to setup a recording studio. Naomba pia outline ya gharama zake (nothing fancy, just a simple studio kwa kuanzia) niweze kujipanga.

Eneo nimeshapata bado mchakato wa ujenzi wa studio yenyewe ila ningependa kufahamu gharama za kusetup studio mpaka ikamilike. Pia kama Mambo yakienda vyema nitahitaji mtu anayeweza kugonga beats na kufanya vocals and mixing ili tuweze kufanya kazi.

Shukrani in advance
 
Unahitaji home studio au proffesional one?

1. Unahitaji kuwa na Computer nzuri yenye spidi nzuri na Ram ya kutosha maana DAWs nyingi ili zipaform mult tracks zinahitaji processor na Ram ya kutosha.

Fanya kutafuta desktop yenye intel core i5 au i7 ya kuanzia 6th Generation. Hutajuta. Pia uwe na 6 Gb of Ram.

Graphic sio issue sana kwenye music production. So utatumia Built in GPU ya pc yako. Price yake sio chini ya 2 Milioni Tsh.

2. Software (DIGITAL AUDIO WORKSTATION)

Hii ni kitu cha Muhimu sana. Sijui nikushauri utumie DAW gani, maana umesema unahitaji Producer. So kila producer ana WORKSTATION aliyo izoea.

Kwa mawazo yangu tafuta Licenced latest FL Studio, Cubese, na pia unaweza ukawa na Daws za Recording tuu kama Adobe audition na Nuendo. Mm nazipenda hizo na nina uzoefu nazo.

Pia itakubidi kununua au kutafuta VST - Virtual Studio technology effects na VSTi Virtual Studio technology instruments.

Hizi ni muhimu sana ili kuzipa nguvu, Effects na Musical instruments DAW zako.

Kama utanunua Genuine unaweza ingia cost ya Mil. Kama 3.5 hivii

Plugins nyingine waweza zipata online kwa ujanja ujanja tuu si lazima ununue

3. MIDI Keyboard
Lazima uwe na Midi keyboard au MIDI controller kwa ajili ya kucheza instruments. Tafuta Keyboard yenye sio chini ya 61 keys ikiwa na multi pads na pitch bender na Modulation wheel.

Ikiwa Full weighetd keys itakuwa poa sana. Waweza check manufacturers kama M- Audio, Yamaha hao wapo vizuri sana.
Depend on your budget unaweza pata kwa 1 - 1.5 Milion.

4. Studio Monitor
Hapa ndio kuna kasheshe. Hizi ni Stereo speaker with build in amplifier kwa ajili ya kupata output ya mziki wako.

Monitor nzuri sio chini ya 2.5 Milion. Kuwa makini sana kwenye hili jambo maani hizi ni muhimu sana kwenye kufanya mastering. Tafuta manufacturers wakubwa kama Yamaha, M-Audio, Precision, wapo na wengine waweza google.

5. Audio interface
Mimi huwa napenda kuita hivyo. Japo unaweza ita Sound card. Hakikisha ina USB 3 pamoja na firewire. Pia iwe na Inputs za kutosha. Hapa napo jikune unavyoweza ukiwa na Budget kubwa ndo utapata nzuri. Ila andaa si chini ya 1.5 milioni.

6. Microphone
for studio Recording tafuta Condenser microphone ni nzuri sana. Kwa live Recording tafuta Dynamic microphone. Unaweza pata kwa elfu 50 tuu. Lakini hakikisha mic zako zina XLR connectors usitumie normal pin ya 2.5"

Tafuta mic ya Rhode au Shure nzuri bei ni kuanzia 1. 5 na stand yake yaweza fika 2Milion

7. Mixer
Kuna mixer aina mbili. a) Powered b) Non power
Tafuta mixer ya kisasa sana ambayo ina njia 4 - 6 tuu iwe non powered ili iwe bei rahisi. Ninavyosema tafuta ya kisasa ninamaanisha. Tafuta ya hadi milioni 2 ila kama budget ipo low waweza fika 1 milioni. Iwe na DSP engine yenye effects za kutosha. Uta enjoy sana

8. Wires, Cords and other cabling
Tafuta nyaya kulingana na setup yako.
Approximately laki 5

NB. Hakikisha una Phantom power kwa ajili ya Microphone yako
 
Unahitaji home studio au proffesional one?
1. Unahitaji kuwa na Computer nzuri yenye spidi nzuri na Ram ya kutosha maana DAWs nyingi ili zipaform mult tracks zinahitaji processor na Ram ya kutosha...
Nashkuru sana kiongozi aisee kumbe mpunga wa maana unahitajika. What if it's just a home studio? Ya kiaina tu

Sent using Jamii Forums mobile app
 
ok

PC WINDOWS (CPU ONLY) core i5 RAM 8GB = laki 7
MIDI KEYBOARD 49 KEYS (M- AUDIO) = Laki 4
CONDENCED MIC =Laki na nusu
STUDIO MORNITORS (M-AUDIO) = Laki 8
SOUNDCARD (M-AUDIO) = Laki 4
FLAT SCREEN LED (32 Inch) = LAKI 4
DAWS (I recommend FL STUDIO, CUBASE AND REASON) = Dont buy!! Go download kwenye torrents unapata full package ni bando lako tu!!!. maana kama kuuzwa zinauzwa kwa dollarss nyingi 300 - 600)

SOUND KITS/SOUND PACKS/ SAMPLES = Zipo online kibaao (DONT BUY THEM unga bando la 5 GB then download)

VST = Go download on torrent sites (nasema tena DONT BUY!!!)

hiyo ndo bei ndogo ya mwisho utayopata kitu bora cha kuanzia kama 2m laki 8 na nusu

NB: Sijajumuisha gharama za wires ndefu za kujitegemea, kiti cha studio (office chair) , mafolonya ya chumba, kopo la cds empty za kuburn
 
Back
Top Bottom