Initially nilijiuliza hivi na hizi picha zote zinazomhusisha na mkuu wa mkoa, inawezekanaje taasisi ya kitapeli ikafanya hivo?
Ila mfumo wao wa ukopaji na urejejeshaji ulinipa shaka, na nilipotaka kuwatembelea ofisini kwao kwa maelezo zaidi (wanadai ni mikocheni) waligoma nisifike, ila tufate taratibu za maombi kadiri ya maelekezo yanayoonekana mtandaoni. Kwa kifupi hawa entertain watu kuwatembelea ofisini, na kwa majibu hayo niliyopewa baada ya kupiga simu kuomba maelekezo ya jengo la ofisi ilipo maeneo hayo, nikajijibu kuwa hata ofisi hawana. Huo mtaa wa bosnia wanaousema kwenye matangazo yao kuwa ndio mahali ofisi ilipo haupo, maana kwa mujibu wa maelekezo yao huo mtaa unaitwa manyara.
Kwa kifupi hao jamaa ni matapeli na ndugu zangu nawasihi pamoja na shida zetu ila tusirubunike kirahisi. Usitume hela kwa mtu usiyemfahamu pasipo kujiridhisha beyond doubts kuwa unazielekeza sehemu sahihi.
Namba zao wameziweka naamini kupitia TCRA hawa watu can be traced easily na wakakamatwa.