Msaada kuhusu diabetic complications kwa mtoto wa mwaka 1 na miezi 4

Kitrack

Member
Dec 11, 2011
50
16
Wanajamvi habari za saa hizi,

Nina mwanangu aliyekuwa na afya nzuri tangu amezaliwa,hajawahi kusumbuliwa na ugonjwa wowote mkubwa zaidi ya mafua ya sikumbili tatu basi.Alikuwa ni mchangamfu na michezo mingi sana kiasi kwamba alipenda pia kula sana.

Wiki iliyopita alianza kunyong'onyea na kuwa mpole baada ya kuanza kutoka rashes kama vile za tetekuwanga kwenye makalio na tumboni upande wa kushoto kuanzia jumapili,jumatatu vikazidi tukampeleka Aghakan tukamwona DR.akamwangalia na kusema ni infections na kumpa antibiotics na dawa ya kupaka.

Hali yake ikazidi kubadilika jumanne akaanza kupumua kwa shida kiasi sio sana kwa vile anatumia dawa tukajua atapata nafuu.Jumatano hali ikazidi kuwa mbaya na homa ikapanda ikabidi arudishwe tena Agakhan na kumuona specialist wa watoto ambaye naye majibu yake hayakutofautiana na Dr.wa mwanzo kuwa ana infections kupitia sikioni na ndio zinamsababishia apumue kwa shida na homa.Tukapewa dawa na kurudi nae nyumbani ikiwa usiku tayari.

Hali ya mtoto ikawa inazidi kuwa mbaya zaidi,kwani alikuwa anakataa kula japo anatamani kabisa kula,anakunywa maji mengi na analia sana.
Baada ya kumpa dawa na kunyonya alilala hadi asubuhi ambapo mtoto alikuwa hoi amelegea anafumbua macho hana nguvu na kutokuweza kuamka.

Ndipo tulipomkimbiza Muhimbili Hospital Emergency pale..alipopokelewa tu ma DR.wakampima damu na mkojo na kugundua kwamba damu yake ilikuwa na very high glucose concentration na mkojo wake hauna sukari kama damu yake.Wakamwekea dripu ya insulin na fluids ilikushusha sukari yake.Hadi ilipofika usiku wake ndio sukari ikaanza kusoma 39.6mmol/l...na kesho yake ikashuka hadi 26..;16.3;hadi kuja kufikia 6..!
wakampima figo,kibofu wakakuta vizima ila kongosho hadi sasa hatujapata majibu sababu regiment ya kufanya kipimo maabara imekwisha.

Akiwa bado amelazwa hapo MNH sukari haijafanikiwa kukaa sawa hata kidogo maana akipimwa asubuhi kabla ya kula utakuta 2.5mmol/l akipimwa saa 4 asubuhi baada ya kula utakuta 7.8-16.3 na jioni hufika hadi 27mmol/l.
Inaniumiza moyo kwa malaika huyu ambaye anasumbuliwa na tatizo hili naomba msaada wa dawa ambazo zitamfanya aweze kupona na sukari yake ikae sawa.

Asanteni.
 
kwa sasa mtoto anaendelea vizuri anaweza kucheza kabisa ,lakini shida iliyopo ni sukari hupanda sana hasa tukimpima usiku 32.4 mmol/l saa 4usiku na 20.5 mmol/l saa 12asubuhi...mchana hushuka hadi 5.7 mmol/l na jioni maranyingi huwa 3.2mmol/l.!wataalamu mliojaliwa na mwenyezi Mungu naombeni msaada nimpeleke wapi na nifanye nini ili hali yake ya sukari isiwe ina badilika sana.Tumechanganyikiwa kwa kweli.
 
Kuna uzi unaitwa kama sikosei "Nakaribisha maswali kuhusu tiba na dawa" wa mkuu geugeosmimi hebu utafute mkuu anaweza akakusaidia mungu akipenda.
 
Pole sana imeniuma hata mm, ila muangalie ni chakula gani mnampa?? Kama vya wanga nying sio nzuri au chakula cha dukani sio mpeni diet ya kiebyeji iandaliwe nyumbani alafu maombi tu ndo dawa weng wanateseka
 
Pole sana mleta uzi, Mungu awatie nguvu kwasababu kiuhalisia wazazi mnawakati mgumu. Chamsingi mfuate ushauri wa Daktari na Mzingatie sana sala na Maombi, majaribu mengine hutokea ili Mungu kuimarisha ukaribu wake wa nyinyi. Usikate tamaa.
 
Asanteni kwa kunipa faraja..vipimo vya pancreatic enzymes vinaonyesha yuko normal..ila hatujaweza kupima beta cells za pancreas..hicho kipimo muhimbili hawana..msaada kwa Dar naweza kipata hospital ipi?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…