Msaada Kuhusu Bima Kubwa ya Gari

Rais Wa Malofa

JF-Expert Member
Aug 27, 2015
683
782
Habari za Mihangaiko wandugu,

Nimekuwa nikisikia shuhuda mbalimbali toka kwa watu kuhusu Bima Kubwa ya Gari ila nimeshindwa kupata muunganikano mzuri wa faida na hasara za Hii Bima.

Je, ni kweli ukiwa na Hii Bima Kubwa Gari yako ikipata ajali au tatizo Kubwa unalipwa na shirika la Bima uliloingia nalo mkataba?

Je, hakuna usumbufu wowote pindi Gari yako ikipata tatizo na ukahitaji kulipwa (endapo wanalipa Kama wanavyojinadi)?

Naomba kwa yeyote mwenye Uelewa na hizi Bima Kubwa za Gari anieleweshe kabla sijajitosa.

Natanguliza Shukrani.
 
Mkuu naomba nikueleze kwa kifupi

Bima kubwa (Comprehensive Insurance) inalinda gari lako kipindi likipata ajali, wizi wa gari, moto na pia madhara/ajali utakayo msababishia mtu (kifo, madhara mwilini na hata uaribifu wa mali)

Chakufanya mtafute mtaalamu akusaminishie gari lako akupe gharama halisi za sokoni za gari lako kwa wakati huu (market price)

Tafuta kampuni inayohaminika juu ya mambo ya bima sikushauri sana upitie kwa mawakala kama ufahamiani nao

Faida ipo kipindi ukipata "mzinga" maana ukichukua gharama ya ulicholipia na utacholipwa (kama ni ajali kubwa) basi we mwenyewe hutaamini

Tatizo tu kuna makato baadhi yatajitokeza wakati wamalipo

Kipindi cha ajali ukiwa na nyaraka zote zitakiwazo ikiwemo zile za polisi basi utalipwa fasta tu.. hakunaga usumbufu kama ukiwa na viambatanishi vitakiwavyo

Angalizo: Usije kabisa ukakatia bima ndogo kama unalipenda gari lako japo pesa imekuwa ngumu kwa tulio wengi
 
Mkuu naomba nikueleze kwa kifupi

Bima kubwa (Comprehensive Insurance) inalinda gari lako kipindi likipata ajali, wizi wa gari, moto na pia madhara/ajali utakayo msababishia mtu (kifo, madhara mwilini na hata uaribifu wa mali)...
Daaaah mkuu somo zuri sana
 
Mkuu naomba nikueleze kwa kifupi

Bima kubwa (Comprehensive Insurance) inalinda gari lako kipindi likipata ajali, wizi wa gari, moto na pia madhara/ajali utakayo msababishia mtu (kifo, madhara mwilini na hata uaribifu wa mali)..

Asante saana kwa ufafanuzi mkuu..
 
Je, kwa kifupi gharama halisi ya comprehensive insurance ni asilimia ngapi ya gharama halisi ya gari lako?

Pia ni kampuni gani ya insurance ambayo ni nzuri kwa huduma zake in general?
 
Je, kwa kifupi gharama halisi ya comprehensive insurance ni asilimia ngapi ya gharama halisi ya gari lako?

Pia ni kampuni gani ya insurance ambayo ni nzuri kwa huduma zake in general?

Kwa uzoefu wangu kwamaana yalishawahi kunitokea garama ni asilimia 3.5 ya bei ya gari yako plus VAT asilimia 18
Kuhusu campany mi nilikata RELIANCE INSUARENCE jamaa hawana longo longo kama una dockment zote j
 
Hebu tufanye nina IST ambayo nimenunua TSH. 10 million. Bima kubwa unaweza kunitoka kiasi gani kwa mwaka.
 
Hebu tufanye nina IST ambayo nimenunua TSH. 10 million. Bima kubwa unaweza kunitoka kiasi gani kwa mwaka.
Premium
= 10,000,000 x 10%
= 350,000/-

VAT on Premium
= 350,000x 18%
= 63,000/-

Total Premium
= 350,000 + 63,000/-
= 413,000/-
 
Back
Top Bottom