Msaada Juu ya kipimo cha HB level test

Jocasta

JF-Expert Member
Aug 28, 2014
474
595
Habari za mwaka mpya ndugu zangu.
JUZI Mrs alikuwa anasumbuliwa na mafua pamoja na kichwa ambavyo vimedumu Kwa mda mrefu Sasa, ikabidi nimpeleke hospitalini.
Alipoeleza dalili hizo Swali la dokta:au una ukimwi?.

Akamwambia inabidi ukacheki damu!!!

Nilipofatilia vipimo alivyofanyiwa nikakuta kapimwa:

1.urine analysis(kama sijakosea)
2.Hb level test
3.Mrdt
Na vyote hakuonekana ana tatizo

Sasa mkanganyiko wangu ni kutokana na swali alilouliza daktari ya Kwimba:au una ukimwi?
Nilidhani alipomwambia ukacheki damu nilitegemea angeenda kupimwa ukimwi Lakini akaandikiwa vipimo tajwa hapo juu.

Ndugu wanabodi Hilo Suala langu limekaaje kitaalamu?msaasa tafadhali!!!
 
Jamani hata mumoja hajachangia
Siku hizi ni kawaida kuulizwa swali kama hilo unapokwenda hospital. Mbona nimewahi kuulizwa hivyo? Kama mara mbili hivi nimeshaulizwa ''umewahi kukutwa na virus wa UKIMWI? Hii inatokana na jinsi unavyoelezea ugonjwa wako, yaani dalili zake.
 
Wanakusanya data nafikiri Kuna mradi fulani.
Huyo Dr ni very unprofessional, hakupaswa kutamka hayo maneno na mpaka wampime ukimwi ni baada ya kuchukua vipimo vingine na kutopata majibu na Hali mgonjwa anaendelea kuumwa
 
Kama ungeenda hospital za serikali hata hawaulizi hayo maswali,yaani wakati unajieleza kwa daktari huku damu inachukuliwa kwaajili ya hiv test. Ni lazima
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom