Msaada juu ya hii kitu (dns.adguard.com)

Vumbi la congo

JF-Expert Member
Oct 26, 2018
666
981
Nilikuwa napata kero ya matangazo online..katika kupekuwa nimekutana na hiyo kitu nikaiweka kwenye setting kama yanavyoelekeza maelekezo naona matangazo sipati tena kwenye zile sites zote ambazo nilikuwa napata kero hiyo..je nauliza pamoja na kwamba matangazo hayaji ipi hasara ya kusett hivyo..yan risk za kusett hivyo ni zipi japo imezuia kweli hayo matangazo?
 
Hasara inayoweza kuwepo ni kwamba sasa tovuti unazotembelea zote zinapitia kwa hao adguard yaani wanaona kuwa unaenda jamiiforums.com ila hawaoni data zozote zaidi ya hapo so kuna uwezekano wa privacy kupotea kiasi fulani kama unajali hayo mambo.

Pia kuna baadhi ya tovuti zinaweza zisifanye kazi sawa kama ukipitia huko.
 
Hasara inayoweza kuwepo ni kwamba sasa tovuti unazotembelea zote zinapitia kwa hao adguard yaani wanaona kuwa unaenda jamiiforums.com ila hawaoni data zozote zaidi ya hapo so kuna uwezekano wa privacy kupotea kiasi fulani kama unajali hayo mambo.

Pia kuna baadhi ya tovuti zinaweza zisifanye kazi sawa kama ukipitia huko.
So wanaweza kuiba password za site nilizo visit?
 
Nilikuwa napata kero ya matangazo online..katika kupekuwa nimekutana na hiyo kitu nikaiweka kwenye setting kama yanavyoelekeza maelekezo naona matangazo sipati tena kwenye zile sites zote ambazo nilikuwa napata kero hiyo..je nauliza pamoja na kwamba matangazo hayaji ipi hasara ya kusett hivyo..yan risk za kusett hivyo ni zipi japo imezuia kweli hayo matangazo?

Kuna njia ya ku block ads without using adguard
 
Ili kujua njia hii inafanyaje kazi kuziba/kuzuia matangazo inabidi kujua kuhusu namna DNS (Domain Name System) inavyofanya kazi, kwa kawaida katika internet ili computer moja iweze kuwasiliana na computer nyingine inabidi kujua anuani yake ya kimtandao (Internet Protocal address au IP address), anuani hizi zipo za aina mbili IPv4 (IP version 4) na IPv6(IP version 6), nitaeleza kwa kutumia IPv4 kwa sababu ndiyo inayotumika sana, anuani za IPv4 zina muundo wa aina x.x.x.x ambapo x ni namba kati ya 0-255 mf. 104.22.6.44, 142.251.37.238, 172.217.170.206. Sasa namba hizi kikawaida ni ngumu kuzishika kwa kichwa ndio maana ikaletwa urahisi wa kutumia anuani kama vile google.com, youtube.com, jamiiforums.com (hizi ndio huitwa Domain Names).

Faida inayopatikana katika kutumia anuani za maneno kama hizi ni kwamba ni rahisi kwa binadamu kukumbuka lakini upungufu wake ni kwamba haziwezi kutambulika na computer kwani computer inatambua namba, hii ni kama vile unavyosave jina la mtu kwenye simu yako ili kurahisha kumtambua mhusika lakini ukipiga simu mtandao unatambua namba sio jina ulilosave. Kwa namna hii basi ukaundwa mfumo wa DNS ili kuweza kuwa kama mkalimani kati ya binadamu na computer (kubadili Domain Name kuwa "IP address") pale binadamu anapotaka kuwasiliana na computer fulani katika mtandao (unapotembelea mf. google.com kiuhalisia unakuwa unawasiliana na computer nyingine inayomilikiwa na Google), kinachofanyika mtu anapotaka kuwasiliana na computer nyingine kwa kutumia DNS ni hivi:

Mtu anaanza kwa kuandika Domain Name kwenye browser yake mf. google.com
  1. Computer inaangalia kwenye faili linaloitwa hosts file. Kwenye linux lipo /etc/hosts, kwenye Windows lipo C:/Windows/System32/drivers/etc/hosts
  2. Ikishindwa kupata kwenye faili la hosts, computer itaangalia kwenye cache (hii ni kumbukumbu ya muda mfupi ambayo computer hutunza inapopata majibu ya Domain Name)
  3. Ikishindwa kupata majibu kwa kutumia njia ya kwanza na ya pili hapo ndipo computer huamua kwenda nje na kutafuta google.com kwa kutumia DNS server ambayo umeiweka kwenye computer kwa mfano wetu huu DNS server ni dns.adguard.com, baada ya kupata majibu, computer hutunza majibu haya kwenye cache ili kukifanyika request ya Domain Name hyo hyo tena iwe rahisi kukumbuka.

NB: Unaweza kuweka configuration na DNS server zaidi moja kwenye computer yako ambapo computer itajaribu DNS server inayofuata iwapo haitapata majibu kwenye ya kwanza.

Hatua hizo zilizoelezwa hapo juu za kutafsiri Domain Names kwenda IP address huitwa Domain Name resolution

Ikiwa computer itafanikiwa kupata tafsiri ya Domain Name (yaani kupata IP address ya Domain Name) basi itaanzisha mawasiliano na IP Address hiyo, kwa hyo computer inaenda kutafuta tafsiri ya jina google.com tu lakini mawasiliano ya vitu kama password n.k vinafanyika baada ya kupata IP address husika na DNS Server haihusiki tena hapo.

Sasa je, hii DNS inasaidiaje kuzuia matangazo?
Kama vile ilivyo kwa watoa huduma wengine wa mtandao, hawa watu wa matangazo pia hutumia majina ya DNS (m.f popads.net) kufikia computer zao (servers) zinazotoa huduma za matangazo na kwa vile ili kufika kwa computer inabidi uwe na IP address na ili kupata IP address ukiwa na Domain Name inabidi uende kwenye DNS server (au faili la hosts)....hapa sasa ndio blocking inapofanyika kwa sababu IP address yoyote itakayopatikana ndio itatumika kufanya connection, kwa hyo kama ikirudishwa IP address ambayo haipo au ya uongo basi computer itaichukua IP Address kama ilivyo na kujaribu kufanya nayo connection ambapo itafeli na hivyo kusababisha kushindwa kufika kwenye server husika, kwa case ya website za matangazo hiki ndio tunachokitaka.

Mfano tuchukulie anuani ya matangazo kama vile popads.net, tutatumia command inayoitwa nslookup (unaweza pia kuangalia dig) ambayo hutumika kuomba tafsiri ya Domain Name kwenye DNS server.

Tutatumia DNS servers ya Google (8.8.8.8) na hii ya dns.adguard.com ili tuone utofauti wa majibu yanayorudi.

1. Ukifanya kwa 8.8.8.8, unapata jibu IP: 216.21.13.13 na 216.21.13.12
nslookup popads.net 8.8.8.8
Code:
Server:     8.8.8.8
Address:    8.8.8.8#53
Non-authoritative answer:
Name:   popads.net
Address: 216.21.13.13
Name:   popads.net
Address: 216.21.13.12
2. Ukifanya kwa dns.adguard.com unapata IP: 0.0.0.0
nslookup popads.net dns.adguard.com
Code:
Server:     dns.adguard.com
Address:    94.140.15.15#53
Non-authoritative answer:
Name:   popads.net
Address: 0.0.0.0
Name:   popads.net
Address: ::
Computer ikiwa inatumia DNS Server ya Google: 8.8.8.8 basi itaconnect kwenye IP ya mtoa matangazo na matangazo yataonekana lakini ikitumia dns.adguard.com itapata IP 0.0.0.0 ambayo sio IP sahihi na hivyo itashindwa kuconnect kwenye server ya mtoa matangazo na kusababisha matangazo kutoonekana.

Je, kuna risk katika kuset hivi?
Binafsi sioni risk kubwa zaidi ya kwamba mmiliki wa DNS server akiamua anaweza kujua ni website gani na gani huwa unatembelea, lakini hii haiepukiki kwani hata kama ukitumia default DNS server ya ISP wako au ya Google bado tatizo lipo pale pale, unachofanya ni kubadili anayeweza kuona hizo taarifa, kama hutaki kutumia DNS server ya mtu itakubidi utumie DNS server yako au kuedit mafaili yako ya hosts kitu ambacho ni kigumu ukizingatia Domain Names zipo nyingi sana na zinazidi kuongezeka kila siku.
 
Back
Top Bottom