Habari wakuu
Mimi nasumbuliwa na tatizo la miguu. Inauma kwenye foot kwa chini upande wa kwenye vidole. Kwa juu hakuna shida wala kurudi kwenye kisigino hakuna shida. Nikitembea juani inakuwa kama inawaka moto na nikiwa sehemu ya baridi kama arusha inakuwa kama inapata ganzi
Ilianza mwaka 1998 baada ya kupata ajali ya gari. Yaliibuka maumivu ya kifua pamoja na miguu. Kifua nilitiwa nikapona. Nimepiga x ray ya mgongo na kiuno wakasema kuna abnormal ndogo tu ambazo haziwezi kusababisha maumivu kiasi hicho
Sasa kesho naenda kuonana na daktari mtalaam wa upasuaji wa viungo kutoka cuba. Naomba maarifa ili niwe na elimu zaidi ya kujieleza na anielewe, maana tupo wengi na tunaweza kuwa na dakika chache kwa kila mmoja
Lakini pia nilikuwa napiga sana punyeto na baada ya ajali nilikuwa kila nikipiga punyeto maumivu yanazidi zaidi
Pia nikipata hofu au mshtuko wowote, maumivu huwa yanaongezeka
Naombeni msaada ili niweze kujieleza vizuri na tuweze kubaini tatizo
Asanteni sana
Nipo Singida