Msaada jinsi ya kudhibiti wizi dukani

IZENGOB

JF-Expert Member
Jun 28, 2014
323
317
Mimi ni mfanya biashara nina maduka mawili,duka moja nakaa mimi duka jingine nimeajiri mtu ambaye anakuwa anauza na kuniletea hesabu kila siku,nafanya hesabu kila baada ya miezi miwili,tatizo ni kwamba dogo ananiibia sana nimekuja kugundua mchezo anaoufanya ni wa aibu,anawaagiza mateja wanamletea balb na taa zingine za umeme ambavyo ni chakavu alafu anavipaki kwenye maboksi nikija kufanya hesabu nakuta kuwa hesabu iko sawa lakini mapato yanapungua na nikikaa mimi mapato yapo.

Mapato ya mwanzo alikuwa anauza mpaka 80,000 kwa siku na sasa kuporomoka mpaka 30,000 kwa siku,ukweli natafuta njia ya kuukomesha wizi huo je nifanyeje?kumtoa siwezi kwani kuna baadhi ya mambo anayoyafanya ni adimu kupata kwa mwingine,anajituma sana anafungua saa 12:30 hana Jumamosi wala Jumapili wala hajawahi kuaga kuwa anaumwa na nilifikiria kufunga CCTV camera nasikia ni gharama kubwa pia mpaka niwe karibu na ofisi ili nipate taarifa kama yupo anayejua CCTV ambazo ni Wiress anijuze,kama kuna njia nyingine nipeni nishauriwe karibuni.!
 
Mkuu ukitaka kumkamata mwizi wako funga cctv bila yeye kujua ilipo na usimwambie kama umefunga cctv mimi nakuambia utashangaa utakachokiona dhidi ya huyo dogo
 
Kama njia anayotumia kukuibia ni hiyo moja ya kubadilisha balbu si umwonyeshe kwamba umeshagundua ? Then, tafuta aina nyingine ya wizi anaofanya !
 
Mkuu ukitaka kumkamata mwizi wako funga cctv bila yeye kujua ilipo na usimwambie kama umefunga cctv mimi nakuambia utashangaa utakachokiona dhidi ya huyo dogo
Sasa duka ambalo Mimi huwa nakaa liko mbali Je kuna uwezekano wa kufunga wirelless CCTV,bei zake inakuaje?
 
Kwanza awe anapumzika hata siku moja kwa wiki, pili lazima aelewe anakuibia, tatu mlipane vizuri ki haki, nne anza kutafuta replacement, huyo tayari kashochoka hapo..
 
Kama njia anayotumia kukuibia ni hiyo moja ya kubadilisha balbu si umwonyeshe kwamba umeshagundua ? Then, tafuta aina nyingine ya wizi anaofanya !
Nimeshamuonyesha but nahisi kuna wizi mwingine anaufanya.
 
Kwanza awe anapumzika hata siku moja kwa wiki, pili lazima aelewe anakuibia, tatu mlipane vizuri ki haki, nne anza kutafuta replacement, huyo tayari kashochoka hapo..
Asante mkuu kwa ushauri wako.
 
kuna jamaa anafunga cctv kwa bei cheee sana,ni fundi tu mzoefu,we unawafuata hawa maprofesional lazima wakupige.kama unataka namba yake nambie nikupe,simpigii debe,ukishindwa achana nae
 
kuna jamaa anafunga cctv kwa bei cheee sana,ni fundi tu mzoefu,we unawafuata hawa maprofesional lazima wakupige.kama unataka namba yake nambie nikupe,simpigii debe,ukishindwa achana nae
Nitumie PM mkuu
 
Eti anafungua jmos n jpili si ndio akupige vizur.jiongeze mkuu pigs chini huyo
 
kuna jamaa anafunga cctv kwa bei cheee sana,ni fundi tu mzoefu,we unawafuata hawa maprofesional lazima wakupige.kama unataka namba yake nambie nikupe,simpigii debe,ukishindwa achana nae
Hizo CCTV anazofunga ni wireless
 
Kama unajua anakuibia nakumfukuza huwezi basi usihangaike na cctv nikazi bure kwakua huwezi kumfukuza cha muhimu mungeze mshahara kisha kanae mueleze ukweli wote kuhusu mchezo wake naamini atabadilika mtu ukimchana na kweli anajijua nitabia anayo ifanya niaibu lazima ataiacha tu
 
Sikia mkuu...haina haja ya cctv ya wireless itakucost sana...wewe funga tu za kawaida ulimradi mlengwa asijue kama kuna cctv humo dukani then unaweka utaratibu wa kila weekend ambayo yeye yupo off unakagua zile cctv kama kuna wizi utabaini tu na hatua zaidi kuhusu mwizi wako zitaanzia hapo.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…