Mwamba wa Dimbani
Member
- Mar 29, 2020
- 6
- 3
Habari za leo,
Ndugu zangu naamini kuna mafundi wazuri tu humu na wazoefu wa masuala ya magari
Nina tatizo ktk gari yangu aina ya Toyota Grand Mark 2 (Gx 110 injini ni 1G kavu). Kwa masiku kadhaa ya wiki iliyopita hapa Dar kulikuwa na mvua sana.
Historia fupi ya tatizo
Sasa kwa maeneo nayokaa kuna madimbwi makubwa mawili nikipita gari inazama hasaaa na tairi nimefunga ni saizi 15 hivyo ipo chini.
Pia nina shamba maeneo ya Mkuranga ndani ndani kdg ambapo huwa naenda sana hasa ktk wakati huu wa mvua kutokana na uwekezaji nilioweka huko. Sasa barabara ukweli zina madimbwi sana makubwa kwa madogo. Kwa masiku ya karibuni imekuwa nikipita kuna taa kwenye dash board inawaka baada ya kutembea.
Nikiizima gari na nikiiwasha tena taa inakuwa imezima. Lakini nikipita tu katika madimbwi inafanya hivi baada ya mwendo kidogo. Je, inawezekana ikawa shida ni maji yameingia katika sensa au injini ina tatizo?
Kuna fundi umeme (hakufanya diagnosis) nilimwendea na kumuuliza akasema ni kwa sababu ya maji tu huenda yanaingia kwenye sensa nisiwe na khofu.
Naomba ushauri wenu.
Naambatanisha na picha niliipiga wakati ilipowaka
Sent using Jamii Forums mobile app