Mrisho Mpoto alaumiwa kwa kumkejeli Padri Kitima Ikulu

Erythrocyte

JF-Expert Member
Nov 6, 2012
126,623
241,469
Msanii asiye na Kipaji , Mrisho Mpoto , amelaumiwa na watu wote kwa kutoa maneno ya kejeli dhidi ya Padri Kitima ambaye pia ni Katibu wa TEC.

Kukejeliwa kwa Padri Kitima kumetokana na kuonekana kwake kwenye hafla ya kusaini mkataba haramu wa Bandari kati ya Tanzania na DP WORLD ya Dubai .

Kauli chafu za Mpagani Mrisho Mpoto alizozitoa hadharani hapo hapo ikulu mbele ya Rais hizi hapa

Screenshot_2023-10-27-20-09-47-1.png


Ikumbukwe kwamba Kitima aliitwa Ikulu kwa njia ya kitapeli ili kumuingiza mkenge , Mwaliko wake huu hapa .

Screenshot_2023-10-27-20-10-37-1.png

Bali kitu ambacho Mrisho Mpoto anapaswa kukielewa ni hiki , Mungu hadhihakiwi , leo anatembea Peku ili awafurahishe wanaomlipa , Lakini kesho aweza kutembelea magoti bila kulipwa .
 
Angetumie Intel Katoliki Vatikaniki.....
na siyo anaanza kulia lia au angesepa baada ya kung'amua ni changa la macho. Sasa hivi ni kama analia lia baada ya kuposwa na mzazi kala mahali. Kilichobakia ni kuhama nyumbani na kwenda kuishi kwa mume.
Mungu ana njia njema zaidi.Angeondoka kwa ghafla ingetafsiriwa vinginevyo.Afadhali aliendelea kuwepo na tumeyajua hadi ya uandishi wa kadi ya mwaliko wa hafla.

cc: walimu wote kuanzia darasa la tatu wapewe sampuli ya kadi kwa ufundishaji mahiri zaidi.
 
Mungu ana njia njema zaidi.Angeondoka kwa ghafla ingetafsiriwa vinginevyo.Afadhali aliendelea kuwepo na tumeyajua hadi ya uandishi wa kadi ya mwaliko wa hafla.
cc: walimu wote kuanzia darasa la tatu wapewe sampuli ya kadi kwa ufundishaji mahiri zaidi.
Padiri Kitima naamini anaishi Dar, sasa lazima alipata mwaliko mapema, halafu kasafiri from Dar to Dodoma kwa ndege saa moja hivi na kwa gari ni kama Km 470 bado hajui anaitiwa nini? Labda yeye ndo alishauri mwaliko uwe hivo ili TEC iendelee kuheshimiwa na kutoonekana walibugi kiharakati?
 
Back
Top Bottom