BINTI anayedaiwa kubanjuka kimalovee na staa wa Bongo Fleva Nasibu Abdul ‘Diamond Platnum’ anayejulikana kwa jina la Irene Hilaly ‘Lynn’ kumbe ni mwanafunzi wa Shule ya Sekondari ya Msimbazi Centre aliyeacha masomo akiwa kidato cha tatu mwaka jana.
Kwa mujibu wa chanzo cha kuaminika, Irene anayeonekana katika video ya Wimbo Kwetu wa Raymond, anadaiwa kuwa na umri chini ya miaka 18, hajahudhuria shuleni tangu Machi mwaka jana na endapo angekuwa akienda, hivi sasa angekuwa kidato cha nne.
“Kila kukicha walimu wanawatuma wanafunzi wenzake wamtafute Irene sababu hawajui pa kumpata, ili tu arudi shule aendelee na masomo kwa kuwa tangu alipofanya mtihani wa kidato cha pili akawa anakuja kwa kusuasua mwisho akakata mguu kabisa ‘form three’ mwanzoni,” kilisema chanzo hicho.
Kaimu Mkuu wa shule hiyo Ahobwile Msimba alisema angependa kumuona na kuzungumza naye ili amalizie masomo yake.
“Tangu kidato cha kwanza kasomo hapa na alikuwa binti mwenye tabia nzuri, kwani mama yake alikuwa akimfuatilia sana maendeleo yake ila baada ya kufariki ndo balaa likaanza, kundi lao walikuwa wanne wote wakawa wanakuja wanapojisikia. Irene alikuwa anavaa sketi ndefu na hijabu ghafla akabadilika na kuanza kuvaa kisketi kifupi na hijabu akaacha,” alisema mwalimu huyo.
Hata hivyo, alisema mwanafunzi huyo hakuwa na maendeleo mazuri shuleni na kwamba hiyo ilimsaidia kuvuka kuingia kidato cha tatu kutokana na kufutwa kwa utaratibu wa mitihani ya kidato cha pili.
“Anatupa wakati mgumu kwa kasi hii ya Magufuli sababu hakutoa taarifa kama kaacha au la, tumekuwa tukimtafuta kwa kipindi kirefu, mara tukaanza kumuona kwenye televisheni na magazeti, tupo tayari aje aendelee na kidato cha nne ili apate cheti kimsaidie maishani maana hata miaka 18 hajafika, au huyo Diamond atusaidie kumpata tuzungumze naye.”
Kaka wa Irene ambaye ndiye meneja wake, aliyejitambulisha kwa jina la Sammy Hilaly amekiri mdogo wake kusoma shule hiyo na kusitisha masomo kwenda kujiendeleza nchini Afrika Kusini.
“Kifupi ni kwamba pale aliacha na kwenda kusoma kozi huko Sauz na ameshamaliza masomo yake,” alisema bila kufafanua elimu aliyosomea.
Source: Tanzaniatoday