Mrejesho: Nimechukua hii LG ya mtumba 49", kuweni makini

Pantomath

JF-Expert Member
Jan 4, 2019
842
3,439
Nilileta uzi hapa kuomba ushauri Tv gani nzuri kwa bajeti ya 500k...

Wachache walisaidia, wengi waliponda bila kutoa msaada, nikaona isiwe tabuu nitumie zangu mwenyewe
Hatimaye nikazama mjini.

Option kama ningechukua mpya, ilikua ni TCL , au Kama ni Hisense basi ni zile za China(boksi jeupe) sio South Africa ambazo ndio zimejaa(boksi la kaki), nilishaambiwa nyingi kisanga, warranty ikiisha nyingi zinaanza maluelue.

Hapo nilisha adjust bajeti mpk 600k, kufika nikazunguka wee, kila nikitaka kupita na mpya akili ina kataa, nikaenda mtaa wanakouza Mtumba, Ilikua ni Sony, Samsung, LG, Phillips, Panasonic, JVC na Sharp kwa uchache.

Kwa mtumba lengo ilikua ni Sony Bravia au LG.

Lengo ilikua size 43"

Sony nikakuta mbili size 43 hio, zote ANDROID, na bei ikawa ipo ndani ya bajeti yangu, kwenda duka jingne Ni Samsung tuu, tena zile zenye camera inc 49-50"

Duka jingne ni JVC tuu, Kwingne ni Sharp.

Duka nililonunulia ndio nikakuta Kuna Samsung, na LG,
Kila nikizungusha kichwa, Jicho linarudi hapa

20230426_095548.jpg


Nilijua kbsa haipo ndani ya bajeti yangu, ila nikauliza, nikaambia 850k, kule nilikokua napita ilikua nikikuta Tv nimeielewa naangalia model # chap napiga picha(hawakatai) naingia kweny mtandao na search.

Kikubwa nilichokua na search haraka ni Mwaka(hata kama ni used ila isiwe imetumika sanaa), iwe Smart, Power consumption, 4K na Size, halafu baadae nikishapata ngapi nzuri nifanye comparisons ni ipi nibebe, hapa ndio ikawa mwisho wa kuchunguza, ikabaki ni chukue ipi? Kati ya 3 ambazo nilizielewa, nikaona nimalizie kwa ku test Speakers, aaah hapa ndio ikafanya hitimisho bila ya kuyumba hii ndio ilikua ya Mwisho lkn ndio ilifanya kazi ya Multiple choice iwe simple, Sikuwaza, nikashushana naye mpk 740k, kibabe sanaaaa, akakubali nikabebaa.

Smart, 4k, 120Hz, IPS, Magic remote control, True black panel, Metalic design, Ultra slim, wide viewing angle, Dalby vision, Ultra Sound Sorround mode, clear voice, Hi-fi Audio, Energy Saving option, e.t.c, e.t.c kwa ufupi nilichotamani nikakosa ni Android tu.

Kwa hili langu niishie hapo, ila nipambane, ingekua pesa sio ya mawazo, hizi shida zote nisinge pata, unaenda Kwenye store za kuaminika, unamwaga mpunga unabeba, Anyway, kwa Leo ndio nipo hapa.

Kwa wanaotaka ANGALIZO

Wafanyabiashara wengine Wahuni sana, kuna Sehemu nilienda kwa hawa wanaouza Mpya Ile sehemu ya size/inch wamebadika ki stika chao kinaonesha inch 42 kumbe ni 40"(nilivyokiona kile ki stika nikajiuliza hapa sio bure kuna kitu, nikakifunua kimya kimya) kampuni nayo haieleweki mana nje haina jina, ila wanadai nayo LG

20230425_120752.jpg
20230425_120757.jpg


Sehemu nyingine Nikakuta LG mpya 720, nikauliza hii kampuni gani? Nikaambiwa LG, nikawauliza Mbona LG mpya ipo chini zaidi ya Hisense? Wakaniambia hizi LG sisi tunaagiza mzigo Mkubwa wa jumla ndio maana hata hapa unaona ni nyingi, kwahio tunapata discount kubwa sabb ni mawakala, Fasta akaiwasha, kucheki kweli imeandika LG, ila akili yangu haikuelewa kbsa.

Nikamwambia naomba remote yake OG, nikaiangalia hamna hata jina la Kampuni(hii sio mistake, ni purposely), nikaangalia hapa kwenye tv Sioni neno LG wala Logo yake, Nikaseme nihitimishe kwa kuangalia nyuma nisome model #, kucheki HAIPO, nakutana na Ile CAUTION tuu tena printed kwenye Housing sio Stica kama ilivyokawaida, 100% nikajua hapa Hamna kituu, kuna jamaa alikuja Fasta akanunua akasepa, huku anaongea, Aisee LG za sikuhizi nyepesii, huyooo.

Mwisho wa yote Japo Brand kwa kiasi kikubwa zina nafasi yake ila ni vizurii tuu kuelewa vitu vya umeme sio vya kuwekea 100% kama umepata kitu cha kudumu daima, Sio kwa sababu Ya JINA au UPYA, ILA kama unaweza kuvizingatia Basi fanya hivyo, hutajilaumu zaidi ya aliyenunua kitu akiwa ANAJUA kbsa kanunua ilimradi.

Kitu kingine katika hizi TV za mtumba, Mimi kwa kusikia kabisa Moja ya wauzaji akimuambia mwenzake aliyekuja kumtaftia mteja kwenye duka la mwenzake "Kama analia njaa, Mpe ile LG ya Kichina"

Kwahio, ukijichanganya ukamini kua vyote mtumba ni OG, imekula kwako..

Ile aliyomuambia ampe ni LG kweli, ila niya China, ambazo Ubora upo chini zaidi ya zile za Korea..

Hili nalo nikalichunguza nikagundua..

Tv OG iliyotengenezwa na kiwanda mama.

Hua wanaandika
Made In Korea/Japani/China/Germany/View attachment 2603031,
Picha Comment #11

Fake au Viwanda vidogo hua wanaandika

Made by Samsung/LG/Sony etc. na ukishaona hivyo ujue ni china.View attachment 2603062
Picha Comment #13

Haikua na Stand zake, nikaweza kwenye hizi za meza za kichina, ikashuka, nika design yangu.
View attachment 2603036
Picha Comment # 10

20230428_163009.jpg
20230428_145438.jpg


Mwenye Uchumi mzuri, Go for brand new,
Mimi wangu umegotea hapo, zaidi ya Hapo nitatembelea rim.
 
Nmenunua samsung 2 mwaka 2013 pale posta kwa wahindi karibu na bank ya azania nmekaa nazo moja nilimgawia rafiki yangu mwaka 2017 nyngne ipo hadi leo. Mwaka 2018 nilinunua lg pale sinza kwenye duka la amazing lifestyle na ipo hadi leo. Hii midude inadumu ila upate brand halisia sio zile zinatengenezwa huko zinapigwa chata tu kwa maelekezo ya mnunuzi.
 
Nmenunua samsung 2 mwaka 2013 pale posta kwa wahindi karibu na bank ya azania nmekaa nazo moja nilimgawia rafiki yangu mwaka 2017 nyngne ipo hadi leo. Mwaka 2018 nilinunua lg pale sinza kwenye duka la amazing lifestyle na ipo hadi leo. Hii midude inadumu ila upate brand halisia sio zile zinatengenezwa huko zinapigwa chata tu kwa maelekezo ya mnunuzi
 
Back
Top Bottom