MREJESHO: Ni nani aliyewapa hawa 'Business permit' badala ya 'Work permit'?

Mhandisi Mzalendo

JF-Expert Member
Aug 23, 2010
6,569
11,152
Habari za muda huu wadau

Naomba niwaletee mrejesho wa mada ya jana kama nilivyopata kutoka kwa mdau wa pale yenye kichwa cha habari

Ni nani aliyewapa vibali vya Business permit badala ya work permit Huawei-tiGO?

Leo asubuhi maafisa wa Uhamiaji walifika ofisi za Huawei-tiGO pale Derm House na kuanza kufanya uchunguzi wao...

Baada ya uchunguzi wa kina na haya ndio yaliyojiri:-

Wamemkamata Zhang Weiquin ambaye ana muhuri wa Namanga, alipoulizwa kama anapajua Kenya akasema hapajui.

Pia amekamatwa mkaburu mwanamke mmoja wa South Africa ambaye ni Head of Technical Assurance for Eastern and Southern Africa ambaye alikuwa na Tour visa, aligongewa alipofika airport.

Wamewachukua hao kama sampling maana wamechuchukua receipts za work permit ambazo wamezilipia kwa ajili ya work permit processing maadam wanaendelea na kazi kabla ya kupewa official work permit.

Kukamatwa kwa wao kimethibitisha kuwa tulichokisema ni uhakika mtupu.

Asanteni sana kwa wote walioshiriki katika zoezi hili kama la task force.

Atleast doctor ameona JIPU lilipo....
 
Baada ya miezi kadhaa kunaweza kuibuka mlipuko wa ajira kwa wasomi wazalendo. Na ni matumaini yangu hili zoezi la kuwakagua wageni walioajiriwa nchini kama wanaendana na matakwa ya kazi wanazozifanya ni endelevu.
 
Tunashukuru kwa mrejesho. Pongezi kubwa pia kwa UZALENDO ulioonyesha. Tuendelee na utafiti wa kuyatambua majipu ili kazi ziendelee na wenye majipu wapangiwe appointment ya kumuona Surgeon General kwa utumbuzi.
 
SA siyo member wa SADC? i think ndani ya hii jumuia visa ziko neutralized!
 
Nimeipenda hii MTU ana Muhuri wa Namanga alipoulizwa Kenya anapajua akasema sipajui.....,hii ndio bongo kila kitu kinawezekana ata kumbeba Twiga kwenye Ndege alafu Mamlaka husika hazina habari.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…