Mrejesho baada ya kuambiwa nichague kati ya Vanguard na Harrier ili ku compensate kama malipo ya kazi

Cheef Baroka

JF-Expert Member
Apr 28, 2019
491
1,010
Kama nilivyowaomba ushauri kwenye post yangu ya 8/1/2021 nikitakiwa kuchagua kati ya gari tajwa hapo juu na kampuni moja ya ujenzi kama fidia ya deni nililowadai kwa muda mrefu bila malipo.

Nawashukuru sana wana Jf na members wa forum hii kwa ujumla kwa mchango wenu wa ushauri , maoni na mawazo kwa ujumla. Na kwa faida ya msomaji mpya ni kwamba Wadau walinishauri nifanye observation ili ku confirm kama zimelipiwa kodi kihalali au zina msamaha wa muda kabda ya kuchagua gari yakuchukua.

Tarehe 11 /1/2021 siku ya j3 nilifika ofisi za TRA kuulizia suala hilo. Nikamkuta dada mmoja (alie barikiwa dharau ya kiwango cha flyover) nikajaribu kumuelezea but hakunipa ushirikiano kabisa ikabidi nitoke kinyonge sana.

Nikapata wazo lakwenda bandari kukagua kwenye importation special book kwa kutumia tar ya gari zilipoingia nchini ili kujua kama ziliingia kwa vibari maalum au ziliingia kama mizigo mingine kawada. Nilibahatikiwa kufika nikamkuta mama mmoja (namshukuru sana) alinipokea vizuri nikamueleza story nzima na nia ya kuja kwangu ofsin kwake.

Bimkubwa akanambia Gari hazijapita pale bandarini na kuhusu usajili na kibari nipeleke plate numbers TRA (kulekule nilikoletewa dharau) pia kuna ofisi kama tatu alinielekeza nifatilie uhalali wa zile gari hapa Tz.

Ikabidi nirudi TRA tar 13 j5 nikakakuta kale kadada tena ikabidi nikakwepe niingie ofis nyingne but nikaambiwa muhusika ni kalekale kadada duh!

Nikaona isiwe kesi nikazama ndani kale kadada kakajifanya hakanijui hakajawahi kuniona ofsini kwake nami nikabadili gia angani nikakaambia nimekuja kama mmiliki wa magari anaetaka kujua tar ya mwisho yakulipia, kakaniomba kadi kakakagua kakasema mbona gari ni za kampuni?

Nikajibu nimekunja sura ko zakampuni hazilipiwi? Kakanambia kamuuliza mke wako, Nikatoka ofsini kwa hasira kwa bahati nikakutana na mwanangu mmoja tulisoma nae Tosamaganga (advance) anaitwa Mudi , nikamuelezea tukio ndo akachukua documents nilizokuwa nazo akazama ndani akapita nukta kwa nukta tukiwa nae ofsn huku kale kadada kakinitazama (mana walikuwa ofis moja japo meza yake ipo mbali sana na mudi)

Mudi kwa mamlaka yake huku akiwasiliana na jamaa zake wa sector zingne husika tukagundua zile gari zliingia nchini kutokea Kenya hivyo ile kampuni imefanya kazi Nakulu kenya kabda yakuja bongo Ila zipo kiuhalali .

Wakuu kama mlivyonishauli nichukue Vanguard so nikawafata kuwaambia kama nachukuwa Vanguard wakanambia nirudishe card ya Harrier nikawapa wakasema kesho tunaitaka kwanza hiyo gari ulochukua nikaona poa tu mana nina kadi yake. Kesho yake nikaipeleka ile gari kufika wakanambia niwaendeshe twende sehem nikawapeleka mara tukafika "Tanroad"

Hapo ndo walipokuja kunivuruga baada yakunambia kuwa zile gari zinatakiwa kubaki under Tanroad na ndo makubaliano ya uingizwaji wake toka bandarini na zina special offer as under government ownership nikawaambia kuhusu deni langu wakasema mtajuana mnalipanaje ila si kwa kumilikishana gari za serikali. Nikaona kuna picha inachezwa mana nimeshapita bandarini gari hazjapita pale afu huku naambiwa mavitu mengne tofauti kabisa .

Kiukweli walinipiga mkwala sana nikaona isiwe kesi nikajifanya mpole nikasema nitawajibu . Nikamfata Mudi nikamuelezea ilivyo akasema pw nimuachie atafte ukweli. Tar 13 / 4 nikiwa moja kati ya ofisi yangu pale ubungo liverside nikakutana na Mudi akiwa na mmoja kati ya wafanyakazi wa "tanroads" ambae alikuwepo kipindi napigwa mkwara jamaa akanichukua tukaenda pale mawasiliano kuna cafe flan kama unashuka stand ya mawasiliano mkono wa kulia .

Jamaa akanipa mchezo wote juu ya ile inshu na ukweli ni kwamba kuna misunderstood kati ya wale jamaa (wachache) wa Tanroad na ile kampuni na ni baada yakujifanya hawataki madili ko wale jamaa wa Tanrd wanawasumbua sana kabda hata ya kumaliza mradi na ndo mana wale wachina wakataka kunipa gari ili kupunguza usumbufu mana wanafatiliwa sana na yote hayo ni baada ya kushindwa kushindwa kuwapa hati mbaya mana ile kampuni pia ni kubwa.

Sasa Mudi na yule mshkaji anaitwa Robart wakasema watanipambania basi mpaka mwezi wa 3 nikawa sijapeleka gari naskilzia tar 25 March nikakutanishwa na boss mmoja wa Usalama nikamuelezea akaja hotel walipo wale wachina akatukusanya akasema hiyo michezo huw ipo na miradi mingi inayofanyika tz baada yakukamilik huwa kuna viongozi hasa wa Tarura na Tanroad huwa wanajigawia baadhi ya mali.

Jamaa akawafata wale jamaa wa tonrd akawapiga mkwara nikawa nimepona hivyo. Chakushangaza Wale wachina wakanirudishia ile Harrier wakataka niwaongezee kama usd3000 wakasema nimewaponeshea vitu vingi pia nimefanya nao kazi kwa uaminifu nakujitoa kwao katika nyakati ngum huku nikiwa silipwi mishahara yangu kwa wakati.
 
Ww uwaongezee tena
 
Aliyekukutanisha na boss wa usalama ni nani na n usalama gani
 
Huyo dada ndio wale Aina wanachelewesha maendeleo ya nchi halafu jiwe alikua anawapa lawama wapinzani,
Tanzania tukiendekeza ujinga Kama huo hatutaendelea kamwe!
Mamlaka nadhani mmepata muongozo uzembe wa huyo dada unalicost taifa ni mzigo Bora arudi kitaa kulea watoto na kudanga maana ndio fani saizi yake


Hili ni povu la buku jero tu!😤😤
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…