Baraza la madiwani katika halmashauri ya wilaya ya Mkalama mkoa wa Singida, limemsimamisha kazi kwa muda usiojulikana mratibu wa Mfuko wa Maendeleo ya Jamii (TASAF), Athumani Dulle, kwa tuhuma za kusajili kaya 28 zisizokuwa na sifa.
Bila kutajwa kiasi kilichotumika kulipa kaya hizo, Dulle amesimamishwa kupisha uchunguzi juu ya tuhuma zinazomkabili.
Pia wa kikao kilichopitisha uamuzi huo, James Mkwega amesema kikao hicho kimewafukuza kazi watumishi watatu wa halmashauri huyo, na kumsimamisha mmoja kwa tuhuma mbalimbali, ikiwemo utoro kazini.
Watumishi hao walioadhibiwa kwa utoro kazini kuwa ni James Kidumo Moses (Ofisa Mifugo Msaidizi), Sera Ogoti (Ofisa Muuguzi), Seleman Ntunga (Fundi Sanifu Maabara
Chanzo: Mwananchi