Mradi mkubwa wa ujenzi wa Bwawa la Kidunda linalojengwa mkoani Morogoro litakuwa na uwezo wa kuhifadhi zaidi ya lita bilioni 190

PendoLyimo

JF-Expert Member
Sep 30, 2014
966
1,053
Mradi mkubwa wa ujenzi wa Bwawa la Kidunda linalojengwa mkoani Morogoro litakuwa na uwezo wa kuhifadhi zaidi ya lita bilioni 190 za maji na kugharimu kiasi cha Shilingi bilioni 336, umefikia zaidi aslimia 27 za utekelezaji wake ambapo mara baada ya kukamilika litasaidia kuboresha upatikanaji wa huduma ya maji katika mikoa ya Dar es Salaam na Pwani.
Akizungumza katika ziara ya Jukwaa la Wahariri Tanzania (TEF) waliotembelea ujenzi wa mradi huo kwa lengo la kujionea hatua iliyofikia ya utekelezaji, Meneja Sehemu ya Mazingira na Uratibu wa Jumuiya za Watumia Maji kutoka Bodi ya Maji Bonde la Wami/Ruvu Janeth Kisoma amebainisha kuwa Bwawa la Kidunda ni miongoni mwa vyanzo vya maji vinavyosimamiwa na Wami/Ruvu huku akieleza mipango iliyopo ya kulitangaza kuwa eneo tengefu.
Aidha Janeth amesema kuwa Bodi imekuwa ikishirikiana na wadau mbalimbali katika kuhifadhi mazingira ambapo mpaka sasa zaidi ya mabirika 29 ya kunyweshea mifugo yameshajengwa kwenye vijiji vinavyouzunguka Mto Ruvu ili mifugo isiweze kuingia mtoni na kuharibu chanzo hicho cha maji.
Naye Kaimu Mtendaji Mkuu wa DAWASA Mhandisi Bwire Mkama amesema kuwa Jiji la Dar es Salaam limekuwa likikutana na changamoto ya upatikanaji wa maji hususani kipindi cha kiangazi hivyo kukamilika kwa bwawa la Kidunda kutakwenda kumaliza kabisa changamoto na kuboresha huduma ya majisafi na salama.
Kwa upande wake, Mwenyekiti wa Jukwaa la Wahariri Tanzania (TEF), Deodatus Balile amesema kuwa vyombo vya habari vimekuwa vikiandaa habari juu ya changamoto ya jiji la Dar es Salaam, hata hivyo vimekuwa vikirejea suluhu ya changamoto hiyo kuwa Bwawa la Kidunda, hivyo mradi huo utakuwa na manufaa makubwa kwa mkoa wa Dar es Salaam.
May be an image of ‎11 people and ‎text that says '‎لسعن l JAMBO τν KIDUNDA KUMALIZA TATIZO LA MAJI DAR ES SALAAM 1:02 f Jambo TV Online‎'‎‎




Like



Comment


Send


Share
 
Back
Top Bottom