Yoda
JF-Expert Member
- Jul 22, 2018
- 48,333
- 69,850
Kwa jinsi mashabiki wa mpira hapa bongo walivyojitolea maisha, akili, hisia, muda na rasilimali zao katika mpira kwa hakika tunaweza kusema mpira ni zaidi ya dini.
Watu wanalala na kuamka wakizungumza mpira, wanashinda wakizungumza mpira.
Jana mchana kwenye East Africa radio kuna kundi la wana Yanga walikuwa wanachangisha pesa za kumpa mchezaji anaitwa Halidi Aucho kwa sababu eti amekuwa hatambuliki kwenye tuzo nyingi nchi hii lakini ni muhimu sana kwa Yanga, hapo wachangiaji ni hadi masikini wenye maisha ya kuunga unga, hii aina tofauti na waumini wa Mwamposa.
Nilikuwa mahali asubuhi kwenye foleni ya huduma, kuna watu watatu pembeni ambao walikuwa hata hawajawanya chai wanajadiliana mkataba wa Kibu Dennis na wanamwagiana details kama vile wanasheria wa mikataba!
Huu mpira bongo kwa hakika umewabamba sana watu, ni zaidi ya dini.